Yametimia Bodi ya Ithibati wanahabari yazinduliwa

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameizindua rasmi Bodi ya Ithibati…
The post Yametimia Bodi ya Ithibati wanahabari yazinduliwa appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameizindua rasmi Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, ambayo imekuwa ikisubiriwa tangu mwaka 2016.
Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 03, 2025 jijini Dar es Salaam, ukiwahusisha wawakilishi mbalimbali kutoka sekta ya habari nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Kabudi amesisitiza kuwa bodi hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha weledi wa taaluma ya uandishi wa habari, kuchochea uwajibikaji, kulinda haki za waandishi wa habari.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau wa habari, waandishi wa habari, pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zinazohusika na sekta ya habari nchini.
Amesema bodi hiyo ni chombo muhimu katika kusimamia viwango vya taaluma ya uandishi wa habari, kuhakikisha uzingatiaji wa maadili ya kitaaluma, pamoja na kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuboresha weledi wao.
Bodi hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229, ikiwa na jukumu kuu la kutoa ithibati kwa waandishi wa habari hapa nchini.
The post Yametimia Bodi ya Ithibati wanahabari yazinduliwa appeared first on HabariLeo.