Waziri Mkuu Mstaafu Pakistan Imran Khan afungwa miaka 14
PAKISTAN : MAHAKAMA nchini Pakistan imemuhukumu Waziri Mkuu wa zamani, Imran Khan, kifungo cha miaka 14 jela kwa…
The post Waziri Mkuu Mstaafu Pakistan Imran Khan afungwa miaka 14 appeared first on HabariLeo.
PAKISTAN : MAHAKAMA nchini Pakistan imemuhukumu Waziri Mkuu wa zamani, Imran Khan, kifungo cha miaka 14 jela kwa tuhuma za rushwa.
Khan, ambaye tayari anashikiliwa gerezani kwa mashtaka ya ufisadi, amekutwa na hatia ya kutumia vibaya nafasi yake kama waziri mkuu.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Nasir Javed Rana katika mahakama iliyoundwa ndani ya gereza alikozuiliwa Khan. SOMA: Tanzania, Pakistan kushirikiana kibiashara
Mwendesha mashtaka, Muzaffar Abbasi, alieleza kuwa mke wa Khan, ambaye pia anatuhumiwa katika kesi hiyo, amehukumiwa kifungo cha miaka saba kwa kumsaidia katika uhalifu.
Wakili wa Khan, Faisal Chaudhry, amesema chama cha Khan kinapanga kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya juu, kikidai kuwa uamuzi huo umechochewa kisiasa.
The post Waziri Mkuu Mstaafu Pakistan Imran Khan afungwa miaka 14 appeared first on HabariLeo.