Wazawa hawimizwa kuchangamkia fursa madini

DAR ES SALAAM: Wazawa waliopo kwenye sekta ya madini wamehimizwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya madini ili kuchechemua na kukuza Pato la Taifa pamoja na uchumi wa mtu mmoja mmoja. Mwenyekiti wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano kwenye Taasisi ya watoa Huduma Sekta ya Madini (TAMISA), Sebastian Ndege amesema hayo leo Mei 14, 2025 …
DAR ES SALAAM: Wazawa waliopo kwenye sekta ya madini wamehimizwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya madini ili kuchechemua na kukuza Pato la Taifa pamoja na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano kwenye Taasisi ya watoa Huduma Sekta ya Madini (TAMISA), Sebastian Ndege amesema hayo leo Mei 14, 2025 na kuongezea kuwa Mei 16 watakuwa na kongamano la kujadili sekta hiyo na vitu mbalimbali litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
Soma zaidi: Mavunde kuongoza kongamano la Madini Geita
Amesema watazungumzia uzinduzi wa kamati yao, kufanya majadiliano kuhusu nafasi ya watanzania kwenye utoaji huduma sekta ya madini pamoja .
Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalilwa amesema wameanzisha taasisi hiyo ili waweze kuwa na taasisi moja hususani kwa wazawa wanaofanya kazi kwenye migodi ili iweze kuwa na tija kwa taifa. Kongamano hili litakalofanyika huu mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
Soma zaidi: Madini Adimu: Chanzo kipya cha migogoro ya kidunia