Watu 12 wafariki kwenye ajali ya barabarani Nakuru

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili Alhamisi jioni baada ya lori hilo kupoteza mwelekeo na kugonga matatu iliyokuwa imejaa abiria, na kuua watu 12 papo hapo.
Baada ya ajali hiyo, kikosi cha waokoaji kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Maafa cha Kaunti ya Nakuru pamoja na maafisa wa trafiki wa eneo hilo walifika katika eneo la tukio na kusaidia kuwaokoa manusura kutoka mabaki ya magari hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamishna wa Kaunti ya Nakuru, Loyford Kibaara, alifichua kuwa lori hilo liligongana na matatu, na kusababisha vifo vya watu 12 huku mtu mmoja akipata majeraha mabaya sana.
Miili ilipelekwa katika mochari ya Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Molo, ambapo inasubiri kutambuliwa na jamaa zao. Wakati huo huo, polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo.
Watu 12 akiwemo mwanafunzi wa shule,walifariki dunia kufuatia ajali iliyohusisha matatu ya abiria na lori katika eneo la Arimi, kwenye barabara ya Njoro-Elburgon, Kaunti ya Nakuru.Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili Alhamisi jioni baada ya lori hilo kupoteza mwelekeo na kugonga matatu iliyokuwa imejaa abiria, na kuua watu 12 papo hapo.