Watoto 48.9% wamedumaa Rukwa

TAKRIBANI nusu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wamedumaa mkoani Rukwa huku kiwango cha udumavu…
The post Watoto 48.9% wamedumaa Rukwa appeared first on HabariLeo.
TAKRIBANI nusu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wamedumaa mkoani Rukwa huku kiwango cha udumavu ni asilimia 48.9 licha ya kuwepo kwa vyakula vya kila aina .
Pia samaki wa aina mbalimbali kutoka Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa na vijito lukuki.
Inaelezwa kuwa chakula sio changamoto mkoani Rukwa kwani ni mkoa wa pili nchini baada ya Ruvuma kwa uzalishaji wa chakula bali kilichokoseka ni elimu ya nini wakazi wa mkoa huu wale.
Haya yamejiri jana wakati Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Chirukile alipokabidhi mifuko 125 ya unga wa mahindi yenye uzito wa kilo 3,025 uliongezewa virutubishi kwa wakuu wa shule za umma 19 za sekondari zilizopo katika Manispaa ya Sumbawanga huku wanufaika ni wanafunzi wapatao 19,779.
Makabidhiano hayo yalifanyika katika Shule ya Sekondari ya Sumbawanga ambapo mifuko hiyo kila mmoja ukiwa na uzito wa kilo 25 yenye gharama ya zaidi ya Sh milioni 3.5 imetolewa na Manispaa ya Sumbawanga ambayo inatekeleza miongozo na Sera mbalimbali ikiwemo mpango wa chakula shuleni na matumizi ya unga wamahindi uliongezewa virutubishi.
Akizungumza katika tukio hilo, Ofisa Lishe Manispaa ya Sumbawanga,Jesca Mwihava anasema manufaa yatokanayo na ungawaji wa unga huo katika shule za Sekondari ni pamoja na kupumguza udumavu na njaa iliyojificha ambapo kwa sasa kiwango cha udumavu ni asilimia 48.9 katika mkoa wa Rukwa.
” Ni shule tano kati ya 35 sawa na asilimia 14 Manispaa ya Sumbawanga zinazotumia unga wa mahindi ulioongezewa virutubishi kupitia wazabuni wanaousambaza shuleni kwa fedha kutoka Serikali Kuu na Ofisi ya Mkurungenzi kupitia mapato ya ndani” anasema.
Huku Mkuu wa Wilaya Chirukile anasema licha ya Watanzania wanasherehekea maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado Manispaa ya Sumbawanga na mkoa wa Rukwa kwa ujumla wake unapambana na maadui watatu maradhi yakiwemo utapia mlo na udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ,ujinga na umaskini.
The post Watoto 48.9% wamedumaa Rukwa appeared first on HabariLeo.