Wasanii wapewa somo kuelimisha jamii

DAR ES SALAAM; Wasanii nchini wametakiwa kutumia filamu na tamthilia kama njia ya kuelimisha jamii, badala ya kuzitumia…
The post Wasanii wapewa somo kuelimisha jamii appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAM; Wasanii nchini wametakiwa kutumia filamu na tamthilia kama njia ya kuelimisha jamii, badala ya kuzitumia vibaya na kupotosha maadili ya kitanzania.
Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Gervas Kasiga ‘Chuma’, ambapo amesisitiza kuwa filamu zikilindwa na kuendelezwa ipasavyo, zinaweza kuibua fursa kwa wasanii, kukuza ajira, na kuongeza pato la Taifa.
“Filamu ni nyenzo muhimu sana katika kujenga taswira ya Mtanzania. Tangu enzi za ukoloni, filamu zimekuwa zikichangia kuibua mijadala muhimu kuhusu jamii yetu,” alisema Kasiga.
Amesema endapo filamu zitakosa mwelekeo mzuri, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii, lakini zikitumika kwa njia sahihi, zitachochea mabadiliko chanya.
Amesema sekta ya filamu ina nafasi kubwa katika kutangaza utamaduni na lugha ya Kiswahili, si tu ndani ya nchi bali hata katika ngazi ya kimataifa.
The post Wasanii wapewa somo kuelimisha jamii appeared first on HabariLeo.