Wasanii wajitokeza tuzo za Injili

WAANDAAJI wa Tuzo za Muziki wa Injili (TGMA) wamesema wametiwa moyo na muitiko wa wasanii wa muziki wa…
The post Wasanii wajitokeza tuzo za Injili appeared first on HabariLeo.
WAANDAAJI wa Tuzo za Muziki wa Injili (TGMA) wamesema wametiwa moyo na muitiko wa wasanii wa muziki wa injili nchini kwa kujitokeza na kutuma kazi zao kwa wingi kwa ajiki ya tuzo hizo.
Hayo yameelezwa leo Aprili 25,2025 na Msemaji wa tuzo hizo, Harris Kapiga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) akielezea hatua iliyofikia katika uandaaji wa tuzo hizo tangu kutambulishwa kwake Februari 7,mwaka huu.
Kapiga amesema kuwa mchakato wa tuzo hizo umefikia asilimia 80 mpaka sasa na siku ya kilele cha tuzo hizo inatarajiwa kuwa Mei 23,mwaka huu na kuongeza lengo la kutoa tuso hizo ni kuwatia moyo wasanii wa muziki wa injili na kwa mwaka huu wamepokea kazi zilizofanywa mwaka 2024 tu.
Akifafanua kuhusu mchakato huo Kapiga amesema baada ya wasanii kupewa nafasi ya kuwasilisha kazi zao zaidi ya 529 walijitokeza kuwasilisha kazi zao kwenye mfumo na ukafanywa mchujo kwa kupiga kura na kupata watu watano katika kila kipengele kwa vipengele 20 vilivyoainishwa.
“Sisi imetutia moyo sana kwa sababu sio watu walikuwa wanakaa na kuchagua watu unajua kuleta kazi ukaingiza kwenye mfumo hiyo jmejitoa muhanga sana lakini kuamini kwa TGMA wanaweza kufanya kitu cha ukweli sisi kwa kazi 529 imetutia moyo sana na hawa waliochguliwa ni ambao walileta kazi,” amesema Kapiga
Baadhi ya vipengele vilivyoainishwa katika tuzo hizo ni wimbo bora wa mwaka ,mtayarishaji bora wa muziki wa injili wa mwaka,mwanamuziki bora wa injili wa mwaka ,wimbo bora ya kusifu pamoja na maeneo mengine ambayo yanaundwwa na majina matano ya washiriki kwa kila kipengele.
Aidha, Kapiga amesema tiketi kwa ajili ya kushuhudia kupongezwa kwa washiriki hao zitapatikana katika tovuti yao na ofisi za Mahali Sokoni zilizopo Kawe na kuongeza kuwa baada ya mchakato wa mchujo katika kila kiprngele kukamilika wasanii watapewa namba zao kwa ajili ya kupigiwa kura ili kupatikana mshindi.
The post Wasanii wajitokeza tuzo za Injili appeared first on HabariLeo.