Wapare wa Taveta walilia kutambuliwa rasmi kama Wakenya

Taifa Leo
Published: Apr 24, 2025 14:56:20 EAT   |  News

JAMII ya Wapare kutoka eneo la Taveta, Kaunti ya Taita Taveta sasa wamepeleka kilio chao bungeni ili kutambuliwa kama Wakenya.

Jamii hiyo inayoishi mpakani mwa Kenya na Tanzania imekuwa ikiishi bila kutambuliwa licha ya kuishi nchini hata kabla ya Kenya kupata uhuru.

Wakiongea mbele ya Kamati ya Bunge, wazee wa jamii hiyo wakiongozwa na msemaji wao Bw Jasper Mruttu, walisema kuwa wamekuwa wakipitia shida kufuatia hali ya kutotambuliwa.

Bw Mruttu alisema kuwa jamii hiyo imekuwa nchini tangu enzi za ukoloni. Hata hivyo, jamii hiyo vilevile inapatikana katika nchi jirani ya Tanzania.

Mbunge wa Taveta, Bw John Bwire alisema kuwa Katiba inatoa mwelekeo ya jinsi serikali inafaa kutambua jamii kama hizo.

"Mipango kama hiyo ni muhimu kwani wataweza kufaidi kama Wakenya wengine. Kuchelewa kwa kutambuliwa kwao ni kinyume cha Katiba," alisema.

Aidha, Spika wa Bunge Bw Moses Wetangula aliitaka kamati hiyo kufanya utafiti ili kunakili jamii zote ambazo bado hazijasajiliwa ili Rais aweze kuzitambua mara moja.

"Kamati hii inafaa kuketi na kutambua makabila yote ambayo hayajatambuliwa. Kabila hizi zina haki ya kukaa nchini na pia kufurahia kama Wakenya wengine," alisema.