“Wanahabari, Wizara ya Elimu Tushirikiane”
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mshikamano na waandishi wa habari hapa nchini umeweza kunyanyua Sekta ya Elimu na kukuza teknolojia. Mkenda amesema hayo leo Novemba 1, 2024 katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC ) uliofanyika mkoani Singida. Mkenda amesema jamii lianza …
The post “Wanahabari, Wizara ya Elimu Tushirikiane” first appeared on HabariLeo.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mshikamano na waandishi wa habari hapa nchini umeweza kunyanyua Sekta ya Elimu na kukuza teknolojia.
Mkenda amesema hayo leo Novemba 1, 2024 katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC ) uliofanyika mkoani Singida.
Mkenda amesema jamii lianza kusema hivi sasa elimu imeshuka kwa kuondoa kutangaza shule bora,mwanafunzi bora lakini jambo hilo kupitia vyombo vya habari wananchi walielezwa.
“Wizara yetu tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano kwani nimekuwa nikitumia vyombo vya habari hata pale kunapohitaji ufafanuzi wa jambo fulani la kielimu hasa linalokuwa na mabadiliko kwenye jami,”
“Mageuzi yote tumeyafanya kwa shule za msingi katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ila elimu ya msingi itakuwa ni lazima katika mtaala mpya hivyo mtoto lazima aanze na amalize,” amesema Mkenda
Mkenda amesema mwanafunzi wa darasa la awali,kwanza na tatu wameanza na mtaala mpya na aliye darasa la pili akiingia darasa tatu ataanza na mtaala mpya na kuendelea mpaka darasa la sita na lazima amalize elimu ya Sekondari najua Serikali inapotekeleza itakuwepo changamoto hakuna kukata tamaa.
Mkenda amesema kutakuwa na mkondo wa amali na ufundi ambapo wakimaliza elimu ya Sekondari watasoma masomo matano na watafundishwa ujasiriamali na mwisho watapata Cheri ambacho atakutumia hata kuomba kazi.
Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya amesema Sekta ya Elimu wamekuwa wakishirikiana nayo kuanzia ngazi ya awali hivyo wataendelea kufuatilia kuhakikisha waandishi wa habari wanapata wasaa kukualika Tena ili waulize maswali.
The post “Wanahabari, Wizara ya Elimu Tushirikiane” first appeared on HabariLeo.