Wanafunzi Geita wahimizwa ubalozi uchaguzi mitaa

Habari Leo
Published: Oct 19, 2024 10:45:59 EAT   |  Educational

WANAFUNZI wa shule za sekondari mkoani Geita wamehimizwa kuwa mabalozi wa kuwahamasisha na kuwaelimisha wazazi wao faida za kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito huo alipotembelea vituo vya uandikishaji katika shule za sekondari Bwela iliyopo wilayani Chato na shule ya Sekondari Siloka …

The post Wanafunzi Geita wahimizwa ubalozi uchaguzi mitaa first appeared on HabariLeo.

WANAFUNZI wa shule za sekondari mkoani Geita wamehimizwa kuwa mabalozi wa kuwahamasisha na kuwaelimisha wazazi wao faida za kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito huo alipotembelea vituo vya uandikishaji katika shule za sekondari Bwela iliyopo wilayani Chato na shule ya Sekondari Siloka wilayani Bukombe.

Shigela anesema iwapo wanafunzi wametimiza umri basi wajiandikishe lakini kwa wale ambao hawajafikisha umri basi washiriki kuwa mabalozi wa zoezi hilo ili liweze kufanikiwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

SOMA: Vijiji 12,333 kushiriki uchaguzi mitaa

Amesema wanafunzi ni wanufaika wakubwa wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani wanapochaguliwa viongozi wazuri watasaidia kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia na hivvo wanapaswa kuhamasisha ajenda ya uandikishaji.

“Tunafahamu wazazi wetu, walezi wetu, wajomba zetu, bibi zetu, babu zetu, wanazo sifa za kuja kujiandikisha, mkirudi muwaulize unajua tunaandikisha kupata viongozi wa vijiji, umejiandikisha, kwa hiyo nyinyi mkawe mabalozi,” amesema.

Aidha Shigela amewahakikishia wananchi wa Geita kuwa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa kwenye vituo vyote vya uandikishaji na hategemei kuona taharuki yeyote inaibuka kwenye vituo hivyo.

“Sisi kama mkoa na wilaya tumeandaa vyombo vya usalama vya kutosha, ili kila mmoja wetu aende kujiandikisha na siku ya kupiga kura, wala asiwe na hofu atakwenda kumchagua kiongozi anayemtaka,” amesema.

Uandikishaji wapiga kura ulizinduliwa rasmi Oktoba 11 na Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambapo unatarajiwa kufikia kikomo Oktoba 20, 2024.

The post Wanafunzi Geita wahimizwa ubalozi uchaguzi mitaa first appeared on HabariLeo.