Wafanyabiashara wakumbushwa kutunza kumbukumbu

Habari Leo
Published: Oct 21, 2024 09:43:48 EAT   |  Business

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara mkoani Kagera kutumia mashine  za kielekroniki kwa usahihi (EFD) pamoja na kutunza vizuri kumbukumbu za taarifa zao za  biashara zitakazowawezesha kukadiliwa kodi kwa usahihi. Akizungumza katika hafla ya utoaji semina elimu ya kodi kwa waandishi wa habari iliyofanyika Manispaa ya Bukoba, Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka …

The post Wafanyabiashara wakumbushwa kutunza kumbukumbu first appeared on HabariLeo.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara mkoani Kagera kutumia mashine  za kielekroniki kwa usahihi (EFD) pamoja na kutunza vizuri kumbukumbu za taarifa zao za  biashara zitakazowawezesha kukadiliwa kodi kwa usahihi.

Akizungumza katika hafla ya utoaji semina elimu ya kodi kwa waandishi wa habari iliyofanyika Manispaa ya Bukoba, Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka Makao Makuu, Hudson Kamoga amesema elimu waliyoipata waandishi hao ni jukumu lao kuirudisha kwa wafanyabiashara.

Kamoga amesema ni muhimu kwa mfanyabiashara kuwa na nidhamu katika kutunza kumbukumbu za biashara kwa manufaa yake.

“Serikali haitaki ulipaji wa kodi usio sahihi hivyo ni vyema kutunza kumbukumbu hizo ili ziwasaidia kudiliwa Kodi kwa usahihi,” amesema Kamoga.

SOMA: Bosi TRA ato Bosi TRA atoa msimamo

Ameongeza kuwa waandishi wa habari ni kiungo muhimu kwani wamekuwa wakiunganisha wananchi katika kupata taarifa na elimu kutoka kwa mamlaka hiyo na kuwa ni muhimu kutumia taaluma yao vizuri Ili kuwafikia wananchi.

Ofisa Elimu na Mawasiliano mkoani Kagera, Rwekaza Joel Rwegoshora amesema wananchi wanatakiwa kulipa kodi kwa hiari ili serikali ikusanye ilivyolenga.

Rwegoshora ameongeza kuwa Mtanzania yoyote anapoanza biashara ndani ya siku 14 anatakiwa kufika ofisi yoyote ya mamlaka hiyo kufanya usajili wa biashara yake ikiwa ni pamoja na kupata TIN namba.

“Mfanyabiashara ana wajibu kutunza kumbukumbu kulipa kodi kwa wakati lakini kusaidiana na mamlaka hii kuwabaini wanaokwepa kulipa kodi,” ameongeza Rwegoshora.

SOMA: TRA kuwaongezea faida wafanyabiashara

“Mamlaka hii inakusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi hivyo hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea bila watu wake kulipa kodi.

Hata hivyo Mossi amewaomba waandishi mkoani Kagera kufikisha elimu kwa umma  hasa kuhusu suala la utoaji wa risti kwani umepungua na kuwa ni muda sasa wananchi kuona umuhimu kudai risti kwani kufanya hivyo ni kutimiza wajibu wao kama mzalendo.

 

The post Wafanyabiashara wakumbushwa kutunza kumbukumbu first appeared on HabariLeo.