Viongozi watakiwa kulinda amani

Habari Leo
Published: Sep 19, 2024 14:17:54 EAT   |  News

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewasisitiza viongozi wa matawi, mashina na serikali za mitaa kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu katika kulinda amani, utulivu na usalama wa taifa letu. Mpogolo amezungumza hayo jana alipozungumza na viongozi wa chama, serikali na wananchi wa kata za Jangwani, Ilala, Upanga mashariki, Mchafkoge, Upanga magharibi, …

The post Viongozi watakiwa kulinda amani first appeared on HabariLeo.

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewasisitiza viongozi wa matawi, mashina na serikali za mitaa kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu katika kulinda amani, utulivu na usalama wa taifa letu.

Mpogolo amezungumza hayo jana alipozungumza na viongozi wa chama, serikali na wananchi wa kata za Jangwani, Ilala, Upanga mashariki, Mchafkoge, Upanga magharibi, Gerezani, Kariakoo, Mchikichini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Wilaya ya Ilala.

Mpogolo amewataka viongozi hao kukemea maovu katika jamii na kuwa mfano mzuri katika jamii na kutoa taarifa pale tu wanapoona watu wanaoleta hofu katika maeneo yao.

“Wapo wengine ambao inawezekana wametumwa kuhakikisha wanakuja kuharibu amani yetu ni vizuri kama viongozi tukakemea kila mmoja kwenye eneo lake lakini pia tukawa askari wazuri kama viongozi tukatoe taarifa kama kuna watu ambao tabia na mienendo yao hatuijui,”alisema Mpogolo.

Ameongeza kuwa amani hiyo na utulivu inaweza kuletwa na umoja na ushirikiano kutoka kwa viongozi wenyewe ambao ni wa chama na serikali kwenda kwa jamii nzima.

Mpogolo amesema utulivu na mienendo yao kama viongozi utasaidia katika kushinda na kupata nafasi ya kuaminiwa na wapiga kura wao kwani sifa kubwa ya wapiga kura ni kuangalia viongozi ni kwa namna gani wanafanya kazi na ushirikiano baina yao ndo njia rahisi ya ufanyaji kazi na utekelezaji wa ilani.

Vile vile, amesema kuwa umoja wao utasaidia kurahisisha uandikishaji wa watu kwenye daftari la wakazi kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwani wakiwa wanafanya kazi kwa pamoja itakuwa rahisi kugawana majukumu na kuhakikisha watu wanajiandikisha kwa wingi.

The post Viongozi watakiwa kulinda amani first appeared on HabariLeo.