Vigogo hawa wataamua hali ya Kenya 2025

Taifa Leo
Published: Dec 30, 2024 07:55:24 EAT   |  News

VIGOGO watano wa kisiasa nchini watabomoa au kujenga Kenya kwa mielekeo watakayochukua mwaka ujao. Wadadisi wa siasa wanasema Wakenya watapiga darubini kila hatua ambayo ukuruba wa Rais William Ruto na waliokuwa mahasimu wake miaka miwili iliyopita Raila Odinga na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuona utakapoelekeza nchi ambayo idadi kubwa ya raia ni vijana wanaolalamikia uongozi mbaya. Kwa upande mwingine, wadadisi wanasema raia watafuatilia kuona iwapo ndoa ya kisiasa ya kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua itaiva na kuvutia wanasiasa wa hadhi upande wao. “Mwaka unapoanza Jumatano ijayo, macho yote yatakuwa kwa vigogo watano wa siasa za kitaifa. Ni mwaka ambao utajaa joto la kisiasa na hatua ambazo watano hao watachukua zinaweza kujenga au kubomoa demokrasia nchini,” akasema mdadisi wa siasa Dkt Isaac Gichuki. Anasema iwapo mkakati wa Rais William Ruto wa kumuondoa Bw Odinga katika siasa za Kenya utafaulu, waziri mkuu huyo wa zamani, akishinda uenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC), siasa za Kenya zitachukua mwelekeo tofauti kuelekea 2027. “Itaaminiwa kuwa Raila hatakuwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2027 na Ruto atawania kurithi ngome za Nyanza, Magharibi na Pwani,” asema Gichuki. Hata hivyo, anasema itategemea na uamuzi wa Bw Raila iwapo atamuunga Ruto kwa muhula wa pili. “Japo Ruto ameteua washirika wa Raila katika mkakati wake wa kurithi ngome za ODM, itategemea na uamuzi wa Raila. Akikosa kushinda na ajitenge na Ruto kuelekea 2027, itakuwa simulizi nyingine. Atakuwa amepangua hesabu ya Ruto,” asema. Wadadisi wanasema uteuzi wa washirika wa Raila katika baraza la mawaziri- Opiyo Wandayi, John mbadi, Wycliffe Oparanya na Hassan Joho, ni mkakati wa Dkt Ruto kurithi ngome za ODM huku kuteuliwa kwa wale wa Uhuru – Mutahi Kagwe, Lee Kinyanjui na kinara wa chama cha Tujibebe Wakenya William Kabogo kukinuiwa kufufua ushawishi wake Mlima Kenya baada ya kung’atuliwa kwa Bw Gachagua.   [caption id="attachment_161534" align="alignnone" width="300"] Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka (kushoto) na Naibu Rais aliyeondolewa Rigathi Gachagua. Picha|Maktaba[/caption] Tangazo la Gachagua Wadadisi wanasema kwa kurejesha ukuruba wake na Bw Kenyatta, Dkt Ruto analenga kuzima umaarufu wa Bw Gachagua ambaye ameahidi kutoa tangazo kubwa kwa wakazi wa Mlima Kenya kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa eneo hilo. Inasemekana Bw Gachagua atazindua chama cha kisiasa ambacho Dkt Gichuki anasema kinaweza kuzua wimbi kali mashinani Mlima Kenya na kunyima UDA cha Dkt Ruto na Jubilee cha Bw Kenyatta ufuasi ambao zimekuwa zikifurahia. “Ikiwa Gachagua atazindua chama na kipate baraka za viongozi wa Gema ambayo imepanuka na kushirikisha Wakamba na iwapo ndoa ya kisiasa na Gachagua itaiva, basi Raila, Ruto na Uhuru watalazimika kuweka mikakati mipya,” anasema Dkt Gichuki.   [caption id="attachment_164525" align="alignnone" width="300"] Rais William Ruto na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta wakisalimiana katika hafla ya kutawazwa kwa Askofu Peter Kimani Ndung’u mjini Embu, mwezi Novemba. PICHA | PCS[/caption] Mchanganuzi wa siasa, Jairu Okemwa, anasema mwelekeo wa kisiasa wa mibabe hawa wa siasa utaamua mustakabali wa taifa mwaka 2025 hasa upande ambao utashawishi vijana. “Kuna uwezekano mkubwa wa vigogo wa kisiasa wanajipanga kugawanya nchi kikabila kama tulivyoshuhudia katika teuzi za hivi majuzi zinazodaiwa kuwa za kupanua Serikali Jumuishi ilhali zinaacha nje jamii na maeneo mengi ya nchi. “Kuna vijana ambao kufikia sasa wamekataa kugawanywa kikabila na ndio wengi na upande utakaowavutia utanufaika,” akasema. Ndoa ya kisiasa ambayo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na aliyekuwa makamu rais Kalonzo Musyoka wanasuka inaonekana kulengwa na ukuruba wa Raila, Ruto na Uhuru ambao wamewatenga. Ukuruba wao unaonekana kuvurugwa kupitia njama kali za mibabe wa siasa za kitaifa na weledi wa kisiasa wa Rais Ruto wa kuzika tofauti zake na Kenyatta.