Tutamfanya Ruto rais wa muhula mmoja, asema katibu wa ODM

Taifa Leo
Published: May 09, 2025 06:55:31 EAT   |  News

SENETA wa Kaunti ya Nairobi, Edwin Sifuna, amesema kuwa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kina nia ya kumfanya Dkt Wiliam Ruto rais wa muhula mmoja. Bw Sifuna, ambaye ni katibu mkuu wa ODM alisema kwamba chama hicho kinalenga kuchukua uongozi kutoka kwa Rais William Ruto kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Sifuna ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ODM wanaokosoa ushirikiano wa chama hicho na serikali ya Ruto anasema kuwa chama hicho cha chungwa kitakuwa na mgombea wa urais katika uchaguzi ujao. “ODM inapigana kutwaa mamlaka kupitia mchakato wa kidemokrasia. Bado tunakusudia, na hatujakata tamaa katika nia yetu ya kuongoza nchi hii. Tutakuwa pale kukabiliana na kila mtu, hata William Ruto,” Bw Sifuna alisema. Aliongeza: “Na matokeo ya kawaida ya hilo ni kwamba tutamfanya awe rais wa muhula mmoja kwa sababu tunataka kuchukua mamlaka kutoka kwake ili tufanye yale tunayoyasema.” Licha ya chama chake kutia saini mkataba wa maeleweno na UDA cha Raisl William Ruto, Bw Sifuna alisema kuwa hajawahi kubadilisha msimamo kuhusu utawala wa Kenya Kwanza. “Maoni yangu hayatawahi kubadilika kwa sababu ninaendelea kupokea habari kwamba, hata katika ziara zake anazosema ni za maendeleo, anakumbana na upinzani mkubwa,” Sifuna alisema Alhamisi asubuhi katika kipindi cha runinga ya Citizen. Alidai kuwa maeneo ambayo yamekuwa yakiunga mkono ODM kwa muda mrefu yamepuuzwa na serikali mbalimbali. “Sisi sote tuliokuwa tunaunga mkono Raila Odinga tumekuwa tukibaguliwa kwa sababu ya siasa. ODM na kiongozi wake Raila Odinga sio kiongozi wa jamii ya Wajaluo pekee. Raila Odinga ni kiongozi wa Kenya. Wafuasi wake, wakiwemo mimi Sifuna ambaye sitoki Nyanza, tumebaguliwa kwa sababu ya msimamo wetu wa kumuunga mkono. Ukienda Pwani, ukienda North Rift. Nilienda hata Baringo, ambako nina mwenyekiti wangu anayeitwa Lekakimon. Anabaguliwa kwa sababu ya kuwa mwenyekiti wa ODM huko Baringo,” aliendelea. Alisema hayo akitofautiana na Seneta wa Kaunti ya Kisumu, Tom Ojienda, ambaye alitetea ushirikiano wa Raila na Ruto kwa kusema unaletea eneo la Nyanza maendeleo. Profesa Ojienda alimtetea Waziri wa Hazina, John Mbadi, dhidi ya madai ya kupendelea eneo hilo ambalo kulingana naye lilitengwa kwa muda mrefu kwa kukumbatia siasa za upinzani. Bw Edwin Sifuna alikuwa amekosoa Waziri Mbadi. “Mara ya kwanza tangu kuanza kwa ugatuzi, Kisumu na Migori zimepokea mgao wa Sh70 bilioni, na sasa tunaona fedha halisi kwa miradi inayoendelea katika eneo ambalo mara chache lilipokea miradi na ambalo lilikuwa limetengwa,” alisema. Ojienda alimtaka seneta wa Nairobi kuunga mkono mipango ya mawaziri inayolenga kufaidi eneo lote la magharibi kwa ujumla.