Tutakulinda kama Wakenya wengine, polisi wamjibu Gachagua

IDARA ya Polisi imemtaka aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoa taarifa kwa polisi kuhusu ratiba na mienendo yake ili kuruhusu maafisa kupanga ulinzi wake ipasavyo.
Kupitia taarifa rasmi, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja alimhakikishia Bw Gachagua kuwa, Wakenya wote wanastahili ulinzi. Bw Gachagua alikuwa amedai kuwa kuna njama ya kumuua.
“Kwa kuzingatia hofu ya usalama aliyotoa Bw Gachagua, anashauriwa kushirikiana na polisi wa viwango vyote iwapo atahitaji ulinzi zaidi na kutoa taarifa mapema kuhusu ratiba na shughuli zake za hadhara ili kuwezesha mipango na uratibu wa kiusalama,” ilisema taarifa ya NPS.
Jumanne asubuhi Gachagua alitoa madai mazito dhidi ya serikali, akisema kuna mpango mahususi uliosukwa wa kutaka kumuua.
Katika barua yake, Gachagua alimlenga moja kwa moja Inspekta Jenerali, akimshutumu kwa kuondoa walinzi wake, hali iliyomweka kwenye hatari tangu alipoondolewa madarakaniHata hivyo, NPS ilisisitiza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwa kuna mikakati ya kuzuia uhalifu.
Bw Gachagua Jumanne alimwandikia barua Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja akilalamikia hatua ya kuondolewa kwa walinzi wake, jambo analosema limemwacha katika hatari ya kuvamiwa na kushambuliwa na na magenge ya wahalifu.
"Una jukumu la kikatiba la kulinda maisha na mali ya kila Mkenya," alisema Gachagua kwenye barua hiyo.
"Hata hivyo, katika hali hii, Bw Kanja, unaendeleza uhalifu na vurugu waziwazi."
Gachagua, ambaye aliondolewa madarakani mnamo Oktoba 2024 kupitia mchakato wa bunge, amedai kuwa maisha yake, ya familia yake na ya wafuasi wake yako hatarini.
Alitoa mifano ya matukio kadhaa ya vurugu ambayo alisema yanahusishwa na njama za kumdhuru.
Alitaja tukio la hivi punde katika kanisa la PCEA Mwiki ambapo walinzi wake wa kibinafsi walilazimika kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya vijana waliovamia ibada. Tukio lingine ni kurushwa kwa kitoa machozi katika mkutano aliohudhuria Desemba 28 huko Nyandarua.
Aliambatisha orodha ya mashambulizi sita aliyodai yalitekelezwa dhidi yake na familia yake tangu Novemba 2024, ikiwa ni pamoja na mazishini Limuru mnamo Novemba 28, 2024 magari yake yalipoharibiwa na waombolezaji kuvamiwa, Shamata, Nyandarua Desemba 28, 2024 ambapo afisa wa polisi anadaiwa kuongoza shambulizi, Kamukunji Grounds, Nyeri – Januari 18, 2025 vurugu zilipozuka wakati wa ibada iliyohudhuria na mkewe, ACK Nyeri mnamo Machi 23, 2025, waumini waliposhambuliwa wakati wa ibada, Naivasha Machi 29, 2025: mkutano wake ulipovunjwa kwa vitoa machozi.
“Kimya chako ni cha kushangaza mno. Hii ni ishara kwamba unakubaliana na kile kinachoendelea,” Gachagua alisema katika ujumbe wake mkali kwa Inspekta Jenerali wa polisi.
Naibu Rais huyo wa tatu wa Kenya alimtaka Bw Kanja kuwafunguliwa mashtaka kwa watu waliohusika na vurugu dhidi yake, kutoa ulinzi rasmi anapohudhuria mikutano ya hadhara, kukomesha kufuatiliwa kwa siri kwa familia yake kunakofanywa na maafisa wa usalama na makazi na mali yake kulindwa.
Gachagua pia alimtahadharisha Inspekta Jenerali Kanja dhidi ya kushirikiana na mabwanyenye wanaoendesha utawala wa mabavu,” akimkumbusha kuhusu Ibara ya 245 ya Katiba ambayo inahusu Polisi kuwa huru na kutoingiliwa kisiasa.
Barua hiyo imenakiliwa kwa Rais William Ruto, Waziri wa Usalama wa Ndani, DCI, NIS, IPOA, Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya na balozi mbalimbali nchini.