Tarakea hawajasahaulika elimu ya fedha

BAADHI ya wajasiriamali, wanafunzi na wananchi kutoka Kata ya Tarakea, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wakiwa katika Ukumbi…
The post Tarakea hawajasahaulika elimu ya fedha appeared first on HabariLeo.
BAADHI ya wajasiriamali, wanafunzi na wananchi kutoka Kata ya Tarakea, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wakiwa katika Ukumbi wa Amcos pamoja na timu ya wataalamu wa Elimu ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake wilayani humo, wakichangia mada mbalimbali kuhusu elimu ya fedha waliyoipata kupitia njia ya filamu.
Mada hizo zina maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha, utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine.
SOMA: Wananchi Ugweno wapewa elimu ya fedha
Filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha ili kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.
Awamu ya tatu ya programu hiyo imeanza kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wajasiriamali katika maarifa ya kifedha katika juhudi za kupanua wigo wa elimu hiyo, ili kuhakikisha maarifa hayo yanawafikia wananchi wengi zaidi wilayani humo.
The post Tarakea hawajasahaulika elimu ya fedha appeared first on HabariLeo.