Tanzania yakaribisha wawekezaji vituo vya kujaza gesi vijijini
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, amesema Tanzania inakaribisha uwekezaji kutoka Uingereza kwa ajili…
The post Tanzania yakaribisha wawekezaji vituo vya kujaza gesi vijijini appeared first on HabariLeo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, amesema Tanzania inakaribisha uwekezaji kutoka Uingereza kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kujaza gesi, hasa vijijini ili kuboresha upatikanaji wa nishati hiyo kwa matumizi ya kupikia kwa gharama nafuu na kwa wakati, hivyo kuchangia katika kuboresha maisha ya wananchi.
Dk Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Marianne Young, katika mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa sekta ya nishati kati ya nchi hizo mbili.
Amepongeza jitihada za Uingereza kusaidia juhudi za Tanzania katika kuboresha upatikanaji wa nishati safi kwa wananchi, hasa vijijini.
SOMA: Mikakati utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia
Kwa upande wake, Balozi Marianne Young ameipongeza kwa Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Afrika wa Nishati akisema hiyo ni hatua muhimu inayothibitisha uongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha upatikanaji wa nishati safi barani Afrika.
Ameongeza kuwa Uingereza itaendelea kuunga mkono jitihada za Tanzania, ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia mashuleni na vijijini.
The post Tanzania yakaribisha wawekezaji vituo vya kujaza gesi vijijini appeared first on HabariLeo.