Tanzania, wadau kuweka kipaumbele usalama wa mgonjwa

Habari Leo
Published: Apr 04, 2025 11:48:46 EAT   |  News

UFILIPINO: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Mkutano wa Saba (7) wa Mawaziri wa Afya ulimwenguni…

The post Tanzania, wadau kuweka kipaumbele usalama wa mgonjwa appeared first on HabariLeo.

UFILIPINO: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Mkutano wa Saba (7) wa Mawaziri wa Afya ulimwenguni kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha usalama wa mgonjwa unapewa kipaumbele kwa kuwa suala hilo ni mtambuka.

Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dk Hamad Nyembea amesema hayo leo Aprili 4, 2025 akimwakilisha Waziri wa Afya, Jenista Mhagama kwenye Mkutano wa Saba (7) wa Mawaziri wa Afya ulimwenguni unaofanyika mji wa Manila nchini Ufilipino, unaolenga kujadili usalama wa mgonjwa.

“Tanzania ina mikakati mbalimbali ya kuhakikikisha usalama wa mgonjwa unapewa kipaumbele ikiwa ni pamoja na uwepo wa miongozo na sera tuliyojiwekea katika ngazi mbalimbali, utumiaji wa nyezo mbalimbali zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kutoholewa nchini,” amesema Dk Nyembea.

Amesema mikakati mengine inayochukuliwa na Tanzania katika kuhakikisha usalama wa mgonjwa ni kusaidia usimamizi wa usalama wa mgonjwa pamoja na uwepo wa mifumo ya ufuatiliaji wa usalama wa mgonjwa.

Amesema mikakati mengine inayochukuliwa na Tanzania katika kuhakikisha usalama wa mgonjwa ni kusaidia usimamizi wa usalama wa mgonjwa pamoja na uwepo wa mifumo ya ufuatiliaji wa usalama wa mgonjwa.

Aidha, Tanzania ni miongoni mwa nchi 27 zilizoshiriki katika mkutano huo sambamba na nchi za Estawini, Micronesia, Gambia, Jamaica, Maldives, Papua New Guinea, Tajikistan, Tuvalu, Angola, Cambodia, Chinese Taipei, Fiji, Georgia, Ujerumani, Indonesia, Japan, Kenya, Libya, Mongolia, Panama, Russia, Slovakia, Sudan Kusini, Timot Leste, Zimbabwe pamoja na Uingereza (UK).

Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “kuwekeza nguvu katika mustakabali wa usalama wa mgonjwa katika utoaji wa huduma za usalama wa afya ya Mgonjwa.” 

The post Tanzania, wadau kuweka kipaumbele usalama wa mgonjwa appeared first on HabariLeo.