TANAPA yakabidhiwa cheti na TBS,chanzo utoaji huduma viwango vya kimataifa

Milard Ayo
Published: Jan 25, 2025 16:57:07 EAT   |  News

Shirika la hifadhi za Taifa hapa nchini Tanapa limekabidhiwa cheti kwa mara ya pili na Shirika la viwango Tanzania TBS Cha umahiri wa mifumo utoaji wa huduma kwa wateja ikiwa ni pamoja na uzingatiaji wa weredi na ubora unaoendana na viwango vya Kimataifa . Cheti hicho ambacho kimekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la viwango […]

The post TANAPA yakabidhiwa cheti na TBS,chanzo utoaji huduma viwango vya kimataifa first appeared on Millard Ayo.

Shirika la hifadhi za Taifa hapa nchini Tanapa limekabidhiwa cheti kwa mara ya pili na Shirika la viwango Tanzania TBS Cha umahiri wa mifumo utoaji wa huduma kwa wateja ikiwa ni pamoja na uzingatiaji wa weredi na ubora unaoendana na viwango vya Kimataifa .

Cheti hicho ambacho kimekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la viwango hapa nchini Dr Ashura Katunzi amesema shirika Hilo limepokea vyeti Saba ambapo vingine ni miongoni mwa vituo ishirini na Moja walivyo navyo huku akisisitiza mashirika mengine kuwa na uweredi katika utoaji huduma .

Dr Ashura amesema utoaji wa cheti hicho umekuwa hauzingatii ukubwa au udogo wa shirika hivyo ni vyema mataasisi mengine yakathibitisha mifumo yao ili kujiweka katika viwango Bora vya utoaji huduma .

Kwaupande wake kamishna wa uhifadhi na maendeleo ya biashara Tanapa Dcc Massana Mwishawa anasema SHIRIKA Hilo litahakikisha kinaendelea Kutoa huduma zenye ubora na viwango vya hali ya juu na vilivyowekwa Kimataifa .

Miongoni mwa vituo vilivyopokea vyeti hivyo ni pamoja na hifadhi ya mkomanzi ambapo Emmanuel mwinara ambaye ni kamishina msaidizi wa uhifadhi na mkuu wa hifadhi hiyo amesema kupewa cheti hicho kwa mara ya pili inawasaidia kujenga imani kwa Umma katika utoaji wa huduma Bora .   

The post TANAPA yakabidhiwa cheti na TBS,chanzo utoaji huduma viwango vya kimataifa first appeared on Millard Ayo.