Taasisi yasisitiza kulinda bunifu mpya

Habari Leo
Published: Dec 21, 2024 10:31:47 EAT   |  General

TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela(NM- AIST) imesisitiza kulinda bunifu mpya zinazoonyeshwa na wanafunzi…

The post Taasisi yasisitiza kulinda bunifu mpya appeared first on HabariLeo.

TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela(NM- AIST) imesisitiza kulinda bunifu mpya zinazoonyeshwa na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili zisiweze kuibwa na wabunifu wengine ikiwemo wahusika kujikwamua kiuchumi.

Aidha taasisi hiyo inahamasisha matumizi ya teknolojia za sayansi,uhandisi ,mahesabu na ubunifu kwa lengo la kuleta mabadiliko mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo nchi ya Tanzania kunufaika nazo

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, anayeshughulikia Taaluma ya Utafiti na Ubunifu kutoka Nelson Mandela, Profesa, Anthony Mshandete wakati wa kufunga kambi ya tano ya mwaka kwa vijana zaidi ya 70 yenye kauli mbiu “Ubunifu kwa miundombinu ya kesho” .

Profesa Mshandete amesisitiza bunifu ni nyenzo zinazoleta mabadiliko katika nchi lakini pia wanafunzi hao wameonyesha bunifu zao hivyo ni lazima mawazo yao yalindwe ili kuhakisha watu hawaibi binifu hizo ili taasisi hiyo iweze kuwajengea uwezo na kuona mali jinsi gani maliakili inakuwa bidhaa

“Serikali inampango mkakati mkubwa katika uendelezaji wa sayansi na teknoloji hivyo bunifu mpya tulizoziona hapa tutazichukua na kuziendeleza ili badae ziwasaidie wanafunzi hawa kuwa bidhaa na kupata ajira maana waneonyesha changamoto za upotevu wa maji,upangaji wa mji, taa za kuongoza magari, vifaa vya watu wasioona ”

Naye Mratibu wa Kongamano hilo la
Sayansi na Teknolojia kutoka Taasisi ya ProjeKt Inspire, Isaya Ipyana amesema kongamano hilo linawapa fursa ya kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha ya kila siku ikiwemo kusadia jamii zaidi kwani sayansi ni ugunduzi na bunifu zinatija zaidi katika kutatua changamoto za kijamii

The post Taasisi yasisitiza kulinda bunifu mpya appeared first on HabariLeo.