Simba, Yanga viwanja tofauti Ligi Kuu leo

Habari Leo
Published: Oct 22, 2024 05:55:58 EAT   |  Sports

MIAMBA ya soka nchini Simba na Yanga leo zinashuka katika viwanja tofauti kusaka pointi 3 muhimu katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanznaia Bara. Bingwa mtetezi Yanga itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. SOMA: Pazia Ligi Kuu bara kufunguliwa leo Yanga imetoka kushinda Karikoo ‘derby’  dhidi …

The post Simba, Yanga viwanja tofauti Ligi Kuu leo first appeared on HabariLeo.

MIAMBA ya soka nchini Simba na Yanga leo zinashuka katika viwanja tofauti kusaka pointi 3 muhimu katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanznaia Bara.

Bingwa mtetezi Yanga itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

SOMA: Pazia Ligi Kuu bara kufunguliwa leo

Yanga imetoka kushinda Karikoo ‘derby’  dhidi ya watani wake wa jadi, Simba Oktoba 19 kwa bao 1-0 katika uwanja wa Benjmain Mkapa, Dar es Salaam wakati JKT Tanzania nayo ilishinda mchezo uliopita ugenini uwanja wa Maj Gen Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam Oktoba 18 dhidi ya Tabora United kwa mabao 4-2.

Yanga ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 15 baada ya michezo mitano wakati JKT Tanzania ni ya saba ikiwa na pointi 10 baada ya michezo saba.

Wekundu wa Msimbazi, Simba itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Simba ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 6 wakati Tanzania Prisons inashika nafasi ya 12 ikiwa pointi saba baada ya michezo saba.

The post Simba, Yanga viwanja tofauti Ligi Kuu leo first appeared on HabariLeo.