Simba Yafunga File la Viporo kwa Kishindo, Yazidi Kuibana Yanga

Mwanaspoti
Published: May 11, 2025 15:33:16 EAT   |  Sports

'FILE' la mechi za viporo ambalo lilikuwa mezani kwa Kocha Fadlu Davids limefungwa rasmi jana Jumapili kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya Simba SC kukamilisha mechi nne kwa mafanikio makubwa kwa kukusanya pointi zote 12. Hii imepunguza tofauti ya pointi kutoka 13 hadi moja dhidi ya vinara wa Ligi Kuu, Yanga SC.