Shakahola ya pili? Wawili wafariki, 57 waokolewa wakizuiwa kanisani

POLISI katika kaunti ya Migori sasa wameanzisha uchunguzi baada ya kubainika kuwa itikadi kali ya kidini huenda ilichangia vifo, msongo wa kiakili na kunyanyaswa kwa waumini wa dhehebu fulani, wakiwemo watoto, eneo la Rongo.
Kisa hicho kilichotokea katika Kanisa la St Joseph Missions of African Church lililoko kijiji cha Kochola, kati ya Kamagambo Mashariki kimeibua hofu ya kutokea kwa maovu sawa na yale yaliyotokea katika msitu wa Shakahola, kaunti ya Kilifi, mwaka jana.
Matukio hayo ya kutia hofu yalianza pale Naibu Chifu wa Kata Ndogo ya Kanyadiedo Abiud Rariende alipopokea ujumbe kuhusu kifo cha kiajabu ndani ya kanisa hilo lisilofahamika na watu wengi eneo hilo.
Mnamo saa kumi na mbili na dakika 25 jioni Jumapili maafisa kutoka vitengo mbalimbali vya usalama wakiongozwa na Naibu Kamishna wa Kaunti walifika katika kijiji hicho kilichoko umbali wa kilomita 10 kutoka mji wa Rongo.
Walipata mwili wa mwanamume aliyetambuliwa kama Francis Muli ndani ya chumba cha maombi kisicho na mwangaza.
Alipatikana amevalishwa joho jeupe na kufunishwa na kitambaa cha rangi ya kijivu.
Maafisa wa uchunguzi walitambua majeraha usoni mwake huku pofu nyeupe ikifuka kutoka mdomoni mwake.
Dalili hizo zilifanya wapelelezi kushuku kuwa huenda alipewa sumu, akanyongwa au kugonjwa na kifaa butu.
Mwili huo ulipelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Rosewood kufanyiwa upasuaji.
Hicho kiilikuwa ni kifo cha pili kutokea katika Kanisa hilo siku hiyo.
Kufuatia ufichuzi huo wa kuhofisha, maafisa wa usalama walifanya msako mkali katika uwanja wa kanisa hilo.
Kile walichopata kiliibua hofu hata zaidi: watu 57, wakiwemo watoto wenye umri mdogo wa miaka mitano, walikuwa wakiishi katika kanisa hilo kwa hali ya kutatanisha.
Baadhi yao walikuwa wamedhoofika kimwili, wengine walionekana kuchanganyikiwa kutofahamu mahala hapo huku wengine wakishindwa kuelezea hali yao kwa ufasaha.
Kundi ambalo liliokolewa lilijumuisha wanaume, wanawake wa umri mbalimbali na wengine wenye mikufu iliyoandikwa “Haleluya” ikiashirikia kuwa walikuwa na itikadi au imani isiyo ya kawaida.
Waathiriwa walisafirishwa hadi Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Rongo kwa ukaguzi wa kiafya.
Lakini kilichoshangaza hata zaidi ni kwamba watu hao wote 57, walikataa kupewa matibabu huku wakilipuka kwa kauli za kidini wakisema uponyaji wa kiroho una nguvu kuliko tiba ya kisasa.
Madaktari walilazimika kuwaruhusu kuondoka kwa sababu waliendelea kuvuruga shughuli za hospitali hiyo.
“Walikataa kushirikiana nasi. Walizua vurugu wakionekana kuamini kuwa wako chini ya maagizo ya kiroho kwamba wasikubali kusaidiwa na madaktari wetu,” akasema mmoja wa wakuu wa hospitali hiyo.
Kundi hilo la watu 57 sasa linazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kamagambo huku maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wakiendelea na uchunguzi (DCI).