Sekondari mpya chachu kupunguza mimba, utoro

Habari Leo
Published: Apr 23, 2025 14:59:08 EAT   |  News

KIGOMA: UJENZI wa shule mpya za sekondari na uboreshaji wa shule hizo unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na…

The post Sekondari mpya chachu kupunguza mimba, utoro appeared first on HabariLeo.

KIGOMA: UJENZI wa shule mpya za sekondari na uboreshaji wa shule hizo unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau unaelezwa kuwa  na mchango mkubwa katika kuondoa changamoto za mimba kwa wanafunzi wasichana na utoro kwa wanafunzi huku ufaulu ukiongezeka.

Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amesema hayo akipokea madarasa mawili ya shule ya sekondari katika shule za Kaphunya na Nyakatundu Wilaya ya Buhigwe mkoani humo.

Meneja masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu akizungumza wakati benki hiyo ilipokabidhi madarasa mawili yaliyojengwa katika shule za sekondari Kaphunya na Nyakatundu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Buhigwe, Michael Ngayarina amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono nguvu za wananchi katika kuanzisha shule mpya za sekondari, kumalizia maboma ambayo hayajakamilika sambamba na kuongeza madarasa katika shule zilizopo kutokana na faida kubwa za shule hizo kwa jamii.

Awali Meneja masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu amesema kuwa benki hiyo imetumia kiasi cha Sh milioni 52 kwa ujenzi wa madarasa mawili katika shule za Sekondari Kaphunya na Nyakitundu Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma sambamba na uwekaji wa madawati kwenye madarasa hayo benki hiyo ikitoa pia jezi seti mbili na mipira mitatu kwa kila shule.

Moja ya darasa lililojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Exim katika Shule ya Msingi Nyakatundu wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma

Kafu amesema kuwa ujenzi wa madarasa hayo unatokana na maombi yaliyowasilishwa kwao na uongozi wa serikali wilaya ya Buhigwe hivyo kupitia mpango wa benki hiyo wa kurejesha kwa jamii (SCR) imeamua kusaidia ujenzi na kwamba uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu ina manufaa makubwa kwa wanafunzi kuongeza ufaulu na kupunguza utoro.

Mmoja wa wanafunzi waliohudhuria makabidhiano hayo, Abisa Pastor kutoka Shule ya Sekondari Kaphunya alisema kuwa kabla ya madarasa hayo walikuwa wanafunzi wa madarasa tofauti wakichanganywa na kusomea daresa moja hivyo uwepo wa darasa jipya utawafanya watenganishwe na taaluma itakuwa kubwa.

The post Sekondari mpya chachu kupunguza mimba, utoro appeared first on HabariLeo.