Sababu za Mlima kutochangamkia urais 2027

Taifa Leo
Published: Mar 23, 2025 05:00:50 EAT   |  News

Muungano mpya wa kisiasa utakaoleta pamoja vyama vilivyoganda katika upinzani unasukwa huku minong’ono ikisema huenda eneo la Mlima Kenya likakosa kuwa na mgombeaji wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Muungano huo utaleta pamoja vyama vilivyobaki katika muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya baada ya ODM kutia saini mkataba wa ushirikiano na serikali ya Kenya Kwanza na viongozi vijana ambao wametangaza kugombea urais, na ambao wametimiza mahitaji ya kisheria kugombea.

Haya yanajiri huku Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee, Jeremiah Kioni, akipuuzilia mbali madai ya baadhi ya viongozi wa chama tawala cha UDA kwamba eneo hilo haliwezi kukosa mgombeaji urais akiyataja kama propaganda duni.

Huku akisisitiza kuwa chama hicho kinachoongozwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kimemteua aliyekuwa waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i kupeperusha bendera katika uchaguzi wa urais mwaka wa 2027, Bw Kioni alisema eneo la Mlima Kenya halitakuwa na mgombeaji wa urais ili kura zisigawanyike.

Katika kauli inayoashiria kuwa kufikia sasa Bw Kenyatta hajazika tofauti zake na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, Bw Kioni alifichua kuwa kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Dkt Matiang’i, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, aliyekuwa Waziri Eugene Wamalwa na Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya.

Kioni pia alipuuzilia mbali uwezekano wa Bw Gachagua kuwa kwenye kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.

“Mtu akishafutwa kazi na Seneti, hakuna mahakama inayoweza kubatilisha uamuzi huo. Gachagua sasa amejiunga na kundi la aliyekuwa Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu, aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko, na sasa Kawira Mwangaza wa Meru ambao kutimuliwa kwao ofisini kuliidhinishwa na Seneti,” alisema Kioni.

Bw Gachagua amekuwa akirai eneo la Mlima Kenya kuungana nyuma ya chama anachotarajiwa kutangaza Mei mwaka huu na pia amekuwa akiashiria kuwa anashirikiana na Matiang’i, Kalonzo, Natembeya na Wamalwa.

Tayari, mbunge huyo wa zamani wa Mathira amezika tofauti zake na kiongozi wa chama cha Peoples Liberation Party (PLP) Martha Karua katika juhudi zake za kuunganisha eneo la Mlima Kenya.

Bw Gachagua amekuwa akisisitiza kuwa eneo la Mlima Kenya litamuunga mgombea urais kutoka jamii za nje ya Mlima Kenya atakayeweza kumuondoa mamlakani Rais Ruto na utawala wake wa Kenya Kwanza.

Kioni alisema Mlima Kenya umeshikilia urais kwa muda mrefu, na sasa unapaswa kuunga mgombeaji kutoka eneo jingine, hasa wale wanaotoka katika jamii ndogo kama Matiang’i.

Afisa huyo aliwataka Wakenya kumuunga mkono Matiang’i, akisema ndiye mtu pekee anayeweza kurekebisha matatizo ya kiuchumi, kisiasa, kiusalama na kijamii yaliyoletwa na utawala wa Rais William Ruto.

“Inawezekanaje rais kutumia muda wake mwingi juu ya magari, akifanya kampeni, badala ya kukaa ofisini kushughulikia changamoto zinazowakumba Wakenya kama usalama, huduma za afya na viwango vya elimu vinavyozidi kudorora?” alihoji Bw Kioni akiwa Nyamira ambako alihimiza wakazi kukumbatia Bw Matiang’i kama mgombea urais wa chama cha Jubilee.

Dkt Matiang’i hajatangaza iwapo atagombea urais na chama atakachotumia iwapo ataamua kujitosa katika siasa. Kwa mujibu wa Kioni, ushirikiano wa kisiasa kati ya Rais Ruto na Bw Raila Odinga hauna maana wala hautadumu kwa muda mrefu.

Hata hivyo, wadadisi wa kisiasa wanasema dalili za mapema zinaonyesha Bw Odinga ataungana na Rais Ruto, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, Spika wa Bunge Moses Wetang’ula na Naibu Rais Kithure Kindiki katika uchaguzi mkuu ujao.

“Sidhani Ruto atamwachilia Raila katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ana ufuasi mkubwa Magharibi na Pwani. Baada ya kutengana na Gachagua Ruto hana budi kuridhia matakwa ya Raila ili agande naye 2027,” akasema mdadisi wa siasa John Kay.