Sababu wenye Diploma kutoswa ajira za Watendaji Vijiji

DODOMA: NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Festo Dugange ameeleza kuwa ajira za Watendaji wa Vijiji katika Utumishi wa Umma hufanyika kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa katika Muundo wa Utumishi wa Kada za Watendaji wa Vijiji/Mitaa uliotolewa na Serikali kupitia Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na.1 wa Mwaka 2013. Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na …
DODOMA: NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Festo Dugange ameeleza kuwa ajira za Watendaji wa Vijiji katika Utumishi wa Umma hufanyika kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa katika Muundo wa Utumishi wa Kada za Watendaji wa Vijiji/Mitaa uliotolewa na Serikali kupitia Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na.1 wa Mwaka 2013.
Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni Mei 22, 2025, Dugange amesema kutokana na masharti hayo wahitimu wa stashahada( Diploma) katika fani tajwa hawawezi kuajiriwa.
“ Ajira za Watendaji wa Vijiji katika Utumishi wa Umma hufanyika kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa katika Muundo wa Utumishi wa Kada za Watendaji wa Vijiji/Mitaa uliotolewa na Serikali kupitia Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na.1 wa Mwaka 2013” amesema na kuongeza kuwa
“Muundo huo umeainisha Watendaji wa Vijiji/Mtaa wanaoajiriwa katika Utumishi wa Umma wanatakiwa kuwa na kiwango cha elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) waliohitimu mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serkali za Mitaa (Hombolo) au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali” amesema Dugange
Ameeleza kuwa kutokana na masharti hayo, wahitimu wa mafunzo ya Stashahada (Diploma) katika fani tajwa hawawezi kuajiriwa kwenye Utumishi wa Umma katika nafasi ya Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kwa kuwa sifa hiyo haijatajwa katika Muundo husika.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Naibu Waziri, Dugange wahitimu wenye sifa hiyo wanaweza kuajiriwa katika Utumishi wa Umma katika Kada nyingine zinazotaja sifa hiyo kama sifa ya kuajiriwa.