Rose Muhando afunika Mtoko wa Pasaka

DAR ES SALAAM; MWIMBAJI wa muziki wa Injili Rose Muhando alikonga nyoyo za mashabiki kwenye Tamasha la mtoko…
The post Rose Muhando afunika Mtoko wa Pasaka appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAM; MWIMBAJI wa muziki wa Injili Rose Muhando alikonga nyoyo za mashabiki kwenye Tamasha la mtoko wa Pasaka lililofanyika usiku wa jana Dar es Salaam.
Rose ambaye watu hupenda kumwita Malkia wa muziki wa Injili aliwainua mamia ya mashabiki waliovutiwa kwa kuimba wimbo wake maarufu kwa sasa wa Amina baada ya watu wote kuinuka na kuimba pamoja na kucheza naye. Kivutio zaidi ni pale alipoamua kuvua viatu ili acheze vizuri kwa kuruka na kutawala jukwaa yeye na madansa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye tamasha hilo amesema anashukuru mashabiki kwa kumtia moyo na kucheza nyimbo zake.
“Tumefurahi sana kwa tamasha hili ni mahali ambapo tunakusanyika pamoja kama waimbaji, nawashukuru mashabiki kwa upendo kwangu Mungu awabariki sana,”amesema.
Wasanii wengine waliofanya vizuri ni Bella Kombo kupitia wimbo wa Mungu ni mmoja alioimba na msanii wa Kenya Evelyn Wanjiru, kundi la Zabroni Singer’s, Paul Clement, Solomon Mukubwa wa Kenya, Harun Laston ‘Zoravo’, Ambwene Mwasongwe, Kwaya ya Neema, Kwaya ya Makuburi, Christina Shusho na wengine wengi.
The post Rose Muhando afunika Mtoko wa Pasaka appeared first on HabariLeo.