Rapa 2 Low ajifyatulia risasi bahati mbaya ndani ya suruali yake kwenye Interview

Milard Ayo
Published: Jan 07, 2025 09:26:41 EAT   |  Entertainment

Msanii wa rap kutoka Texas, 2 Low amenusurika kujijeruhi baada ya Bunduki yake iliyokua mfukoni mwake kufyatuka ghafla wakati wa mahojiano ya moja kwa moja kwenye kipindi cha YouTube, One on One with Mike D ambapo Msanii huyo alikuwa akijadili safari yake ya muziki. Bunduki hiyo ilifyatuka ghafla alipokuwa akiweka mkono mfukoni hali iliyosababisha mshangao […]

The post Rapa 2 Low ajifyatulia risasi bahati mbaya ndani ya suruali yake kwenye Interview first appeared on Millard Ayo.

Msanii wa rap kutoka Texas, 2 Low amenusurika kujijeruhi baada ya Bunduki yake iliyokua mfukoni mwake kufyatuka ghafla wakati wa mahojiano ya moja kwa moja kwenye kipindi cha YouTube, One on One with Mike D ambapo Msanii huyo alikuwa akijadili safari yake ya muziki.

Bunduki hiyo ilifyatuka ghafla alipokuwa akiweka mkono mfukoni hali iliyosababisha mshangao kwa Mtangazaji na Waomgoza kamera ambapo Mtangazaji Mike D aliuliza nani amepigwa risasi huku 2 Low akionekana kushtuka na kutoa sehemu ya Bunduki hiyo kabla ya kuirudisha mfukoni.

Baada ya tukio hilo 2 Low alihakikishia kila Mtu kuwa yuko salama na alisema kwa utani kuwa “Natumaini niko sawa,” alipokuwa akitazama mguu wake ambapo Katika video iliyofuata Mtangazaji Mike D alisema “karibu ajipige risasi mwenyewe kwenye kamera lakini tunashukuru kila Mtu yuko salama.”

The post Rapa 2 Low ajifyatulia risasi bahati mbaya ndani ya suruali yake kwenye Interview first appeared on Millard Ayo.