Rais Samia azindua Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi

Mtanzania
Published: Oct 04, 2024 16:32:42 EAT   |  News

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kumekuwa na malalamiko yanayogusa mfumo wa kodi kwa ujumla kutokana na wafanyabiashara na wananchi kudai kuwepo kwa wingi wa kodi, tozo na viwango vya kodi visivyo rafiki na jinsi kodi hizo zinavyokusanywa. Ameyasema hayo leo Oktoba 4,2024, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Tume ya […]

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kumekuwa na malalamiko yanayogusa mfumo wa kodi kwa ujumla kutokana na wafanyabiashara na wananchi kudai kuwepo kwa wingi wa kodi, tozo na viwango vya kodi visivyo rafiki na jinsi kodi hizo zinavyokusanywa.

Ameyasema hayo leo Oktoba 4,2024, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi ambapo ameagiza tume hiyo kuliangalia kwa kina na kuja na maboresho.

“Baadhi ya wafanyabiashara wanalalamikia wingi wa kodi na tozo lakini pia viwango vya kodi kutokuwa rafiki na hii ni kawaida, unajua Mtu ana hiyari kwenda kulipa faini bila kulazimishwa mwenyewe kwasababu faini ni kodi inayotokana na kosa, kwahiyo mtu analipa ili asiende jela lakini kodi tunayoizungumzia hapa ni kodi inayotokana na kitu kizuri”

“Kuna malalamiko ya weledi kutozingatiwa wakati wa kukusanya kodi, mfano matumizi ya nguvu, lugha zisizo na staha na ubabe kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali na baadhi ya biashara kutozwa kodi au tozo zinazoshabihiana na Taasisi zaidi ya moja kwahiyo hapa napo kuna mashakamashaka ambayo inatakiwa yakatazamwe,” amesisitiza.