Rais Samia ala chakula na waokoaji wa Kariakoo
Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Januari 30, 2025 amekula chakula cha mchana pamoja na walioshiriki uokoaji katika jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo Novemba 2024. Katika hafla hiyo ya chakula cha mchana, Rais Samia amezungumza mambo mbalimbali, huku akimtaka Waziri wa Biashara kuangaliwa suala la wageni kufanya biashara inayofanywa na wenyeji. “Haiwezekani […]
Na Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Januari 30, 2025 amekula chakula cha mchana pamoja na walioshiriki uokoaji katika jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo Novemba 2024.
Katika hafla hiyo ya chakula cha mchana, Rais Samia amezungumza mambo mbalimbali, huku akimtaka Waziri wa Biashara kuangaliwa suala la wageni kufanya biashara inayofanywa na wenyeji.
“Haiwezekani mgeni akawe mmachinga, vijana wetu watafanya kazi gani, kwa hiyo waziri wa biashara simamia hilo,” amesema Rais Samia.
Aidha ameeleza kuwa kupitia mradi wa DMDP, wamejipanga kujenga soko lingine zuri kama lilivyo la Kariakoo katika eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam, hivyo baadhi ya wafanya biashara watahamishwa kwenda kwenye soko hilo.
Kuhusu kuporomoka kwa jengo la Kariakoo, amesema
kumewapa somo na huenda mali zinazofichwa humo hazilipiwi kodi.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema Kamati maalumu iliyoundwa kuchunguza kuporomoka kwa jengo la Kariakoo na kufanya ukaguzi wa kina wa majengo yaliyopo katika eneo hilo imekamilisha kazi yake na imewasilisha taarifa itakayokabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.