Rais Samia aibeba Simba Sauzi, agharamia malazi, usafiri

Mwanaspoti
Published: Apr 23, 2025 08:49:34 EAT   |  Sports

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameipa Simba sapoti ya usafiri wa kwenda Afrika Kusini na kugharamia malazi kwa timu hiyo katika kipindi chote itakapokuwa huko kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch, Aprili 27, 2025.