Rais Chapo kuwasaidia raia 1,000 wa Msumbiji
MSUMBIJI : RAIS wa Msumbiji, Daniel Chapo, ameamua kuwasaidia raia 1,000 wa Msumbiji wanaozuiliwa nchini Afrika Kusini kwa…
The post Rais Chapo kuwasaidia raia 1,000 wa Msumbiji appeared first on HabariLeo.
MSUMBIJI : RAIS wa Msumbiji, Daniel Chapo, ameamua kuwasaidia raia 1,000 wa Msumbiji wanaozuiliwa nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na uchimbaji madini haramu.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Rais Chapo alisema utawala wake unalenga kuboresha hali ya uchimbaji madini nchini Msumbiji ili kuwazuia vijana kutoka nchini humo kuvuka mpaka kwenda Afrika Kusini na kuhatarisha maisha yao katika operesheni hatari na zisizo halali.
Rais Chapo pia alisisitiza umuhimu wa kuzingatia makubaliano ya kihistoria ya kazi kati ya mataifa hayo mawili, akiongeza kuwa serikali yake itaunga mkono tu taratibu za kisheria za uchimbaji madini.
SOMA: Wachimbaji madini walazimika kula nyama ya binadamu, mende
Mzozo kati ya mamlaka ya Afrika Kusini na wachimba migodi haramu ulitokea katika mgodi uliotelekezwa huko Stilfontein, ambapo vifo vya watu 70 viliripotiwa, na wachimbaji madini haramu 1,500, wengi wao wakiwa raia wa Msumbiji, walikamatwa.
The post Rais Chapo kuwasaidia raia 1,000 wa Msumbiji appeared first on HabariLeo.