PPRA yatakiwa kusimamia uadilifu matumizi ya fedha

Habari Leo
Published: Feb 21, 2025 10:25:31 EAT   |  Business

NAIBU Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Mrope amewaagiza wafanyakazi wa mamlaka ya…

The post PPRA yatakiwa kusimamia uadilifu matumizi ya fedha appeared first on HabariLeo.

NAIBU Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Mrope amewaagiza wafanyakazi wa mamlaka ya Udhibigi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kusimamia matumizi ya fedha na mali kwa kuzingatia uadilifu na maadili.

Mrope aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Tano wa Baraza la Nne la wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA) lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julia’s Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.

Amesema watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waadilifu muda wote sambamba na kusimamia matumizi ya fedha na mali za umma pindi wanapotoa huduma hatua ambayo itasaidia kudhibiti matumizi ya ovyo.

“Watumishi wa Umma pia mnawajibu mkubwa wa kuepuka vitendo vinavyoweza kushawishi kutenda yaliyo kinyume na maadili wakati mkiendelea na majukumu yenu, watumishi wa umma kwa nchi nzima ni zaidi ya laki sita ila wananchi ni zaidi ya milioni 60 kwa mantiki hiyo naona mlivyo na kazi kubwa ya kulinda maslah ya wananchi,”amesema.

Aidha amesema mabaraza ya kazi ni sehemu ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo changamoto za kazini ambayo pia yanachangia kupunguza migogoro na migongano sehemu za kazi na kwamba changamoto zitakazoibuka zitumike kama frusa kutagua shiva za wafanyakazi.

“Mabaraza ya kazi ni kujadili changamoto zenu, kadhalika mnatakiwa kuwa mfano katika utendaji wenu wa kazi endeleeni kutoa maelekezo kwa uwazi yawe sahihi kwa kuzingatia uadikifu,” amesema.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa Baraza hilo kujadili namna bora ya kuzijengea uwezo Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali hatua ambayo itasaidia kupata uelewa kuhusiana na matumizi sahihi ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.

“Kuna mambo mengi mmeanzisha ikiwemo mfumo wa kieletroniki wa kuendelea kufanya ununuzi kwa njia ya mfumo wa kieletroniki ( NEST) yoeni nafasi kwa wadau wenu wafahamu mifumo yenu vizuri”alisema

Awali katika mkutano huo Mkurugenzi wa (PPRA) Dennis Simba amesema tangu kuanza kwa mfumo wa manunuzi ya Umma Nest tayari umeunganishwa na mifumo 20 kuendana na malengo ya serikali ya kuhakikisha mifumo inasomana kwa lengo lakuweka uwazi zaidi.

Adiah amesema changamoto kubwa wanayokabilinana naho ni ukosefu wa watumishi wa kutosha jambo linasababisha baadhi ya kazi kitokwenda kwa kasi inayotakiwa.

The post PPRA yatakiwa kusimamia uadilifu matumizi ya fedha appeared first on HabariLeo.