Polisi kuimarisha usalama uchaguzi mkuu 2025

ZANZIBAR: JESHI la Polisi limeeleza kuwa limejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu. Kauli…
The post Polisi kuimarisha usalama uchaguzi mkuu 2025 appeared first on HabariLeo.
ZANZIBAR: JESHI la Polisi limeeleza kuwa limejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Intelijensia ya Jinai wa Polisi (CP), Charles Mkumbo, wakati wa kikao kazi cha 20 cha Maofisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano wa Serikali, kilichofanyika Zanzibar.
Katika hotuba yake, Kamishna Mkumbo amewataka maofisa habari kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha usalama wa uchaguzi. Aidha, amewataka kuepuka kutoa taarifa za uchochezi au udanganyifu ambazo zinaweza kusababisha mihemko na vurugu kwa wananchi.
Pia, Kamishna Mkumbo amewahimiza maofisa habari kuzingatia weledi na ukweli wa taarifa wanazotoa, akisisitiza kuwa wanalo jukumu la pamoja la kulinda usalama wakati wa uchaguzi. Alibainisha kuwa uwepo wa amani na utulivu ni nguzo muhimu inayochangia uchaguzi kufanyika kwa mafanikio.
Jeshi la Polisi limeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa mazingira ya uchaguzi yanakuwa salama, huku likisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa vyombo vya habari katika kuelimisha wananchi kuhusu amani na utulivu wakati wa uchaguzi.
The post Polisi kuimarisha usalama uchaguzi mkuu 2025 appeared first on HabariLeo.