Papa Leo XIV alikuwa ametajwatajwa kuchukua ‘uongozi wa mapema’ uchaguzini

MOSHI mweupe ulitoka kwenye paa la Kanisa la Sistine Chapel Vatican jijini Roma Alhamisi jioni kutangaza kuchaguliwa kwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki lililo na wafuasi zaidi ya 1.4 bilioni kote duniani.
Kadinali Robert Prevost kutoka Amerika, mwenye umri wa miaka 69 alichaguliwa kumrithi Papa Francis aliyefariki dunia Jumatatu ya Pasaka mwaka huu akiwa na umri wa miaka 88 na kuzikwa siku saba baadaye.
Alichagua jina la Papa Leo XIV na kuwa kiongozi wa 297 wa Wakatoliki duniani.
Umati katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican ulilipuka kwa shangwe huku kengele zikilia kutoka kwenye kanisa kuu la Vatican, kuthibitisha kwamba makadinali 133 waliokuwa wakishiriki uchaguzi tangu Jumatano walikuwa wamefikia uamuzi wa theluthi mbili kuhusu mrithi wa Papa Francis.
Kufikia mwisho wa duru ya tatu Alhamisi mchana, hakuna aliyekuwa amepata theluthi mbili ya kura za makadinali, hivyo moshi ulikuwa mweusi.
Moshi mweusi wa kikao cha upigaji kura asubuhi ulionekana saa sita na dakika hamsini mchana saa za Kenya, kisha makadinali walichukua mapumziko ya chakula cha mchana.
Hii ilikuwa mara ya pili kuonekana kwa moshi mweusi, baada ya ule wa kwanza kuonekana Jumatano usiku. Hii ilimaanisha kuwa katika duru tatu za mwanzo, hakuna aliyekuwa amewashawishi makadinali 133 wapige kura kumchagua.
Tangazo hilo lilisubiriwa kwa hamu duniani kote, huku waumini wengine wakifika Uwanja wa Mtakatifu Petro kushuhudia wenyewe ishara hiyo.
Hakuna papa aliyewahi kuchaguliwa katika duru ya kwanza, hivyo moshi mweusi wa Jumatano haukushangaza. Papa Francis, papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini, alichaguliwa jioni ya siku ya pili ya mkutano wa uchaguzi mwaka 2013, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Benedic XVI, mwaka 2005.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa papa mpya Leo XIV. Ulimwengu ulipokuwa ukisubiri ishara ya moshi mweupe, shirika la Reuters liliripoti kwamba alikuwa mmoja wa makadinali tisa waliokuwa “wakitajwa” kuongoza uchaguzini.
Mwingine alikuwa Kadinali Jean-Marc Aveline, mwenye umri wa miaka 66 kutoka Marseille. Anajulikana kwa tabia yake ya urahisi, ucheshi na ukaribu wa kiitikadi, hasa kuhusu uhamiaji na mahusiano na Uislamu.
Mwingine alikuwa Kadinali Charles Maung Bo, mwenye umri wa miaka 76 kutoka Myanmar. Uteuzi wake katika nchi yenye wafuasi wengi wa dini ya Kibudha uliangaziwa sana mwaka 2015.
Hata hivyo, Bo ni mtu wa kutofautiana mitazamo nchini mwake — hata ndani ya wachache Wakatoliki — kutokana na mahusiano yake na uongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, uliochukua mamlaka tangu 2021.
Jina lingine lililotajwa lilikuwa la Kadinali Peter Erdo, mwenye umri wa miaka 72 kutoka Hungary.
Uteuzi wake ungetazamwa kama wa maelewano, kutoka kwa kambi ya kihafidhina lakini aliyejenga daraja na mtazamo wa maendeleo wa Franciso Kardinali Erdo alizingatiwa pia mwaka 2013 kwa kuwa na uhusiano mpana barani Ulaya na Afrika.
Kadinali Mario Grech, mwenye umri wa miaka 68 kutoka Gozo – kisiwa kidogo sehemu ya Malta – naye alitajwa kuwa na ushawishi. Alionekana awali kuwa wa kihafidhina, lakini sasa anashikilia ajenda ya mageuzi ya Papa Francis.
Kadinali Cristobal Lopez Romero kutoka Morocco pia alizingatiwa.
Askofu mkuu huyu wa Rabat aliyezaliwa Hispania, mwenye umri wa miaka 72, anajulikana kwa kazi ya huduma na utetezi wake wa wahamiaji. Hata hivyo, amewahi kusema wazi kuwa hataki kuwa Papa.
Kadinali Pietro Parolin, Muitaliano mwenye umri wa miaka 70, alionekana kuwa mgombea wa maelewano kati ya wahafidhina na wenye mitazamo ya maendeleo.
Amekuwa mwanadiplomasia wa Kanisa kwa muda mrefu na amehudumu kama katibu mkuu wa Papa Francis tangu 2013. Nafasi hii hufananishwa na waziri mkuu, na mara nyingine huitwa “naibu papa” kwa kuwa ndiye wa pili kwa mamlaka Vatican.
Kadinali Robert Prevost ametumia muda mwingi wa maisha yake kama mmishonari Peru na hajulikani sana kimataifa. Alitokea Chicago na amewavutia makadinali wenzake kwa mtindo wake wa kimya.
Kadinali Luis Antonio Tagle mwenye umri wa miaka 67 kutoka Ufilipino pia alikuwa ametajwa. Amekuwa akijulikana kama “Francis wa Asia” kwa sababu ya tabasamu lake rahisi na kujitolea kwake kwa haki ya kijamii.
Katika hatua iliyoonekana kama njia ya kumpa uzoefu wa Vatican, Papa Francis mwaka 2019 alimteua kuwa mkuu wa kitengo cha kimishonari cha Kanisa.
Mgombea mwingine alikuwa Kadinali Matteo Maria Zuppi, Muitaliano mwenye umri wa miaka 69 anayeitwa “padri wa mitaani.”
Analenga wahamiaji na maskini, na si mtu wa kupenda sherehe na heshima. Anajulikana kama “Padre Matteo,” na huko Bologna ambako ni askofu mkuu, mara nyingi hutumia baiskeli badala ya gari rasmi.
“Mapapa 10 wa hivi karibuni walichaguliwa wakiwa na wastani wa umri wa miaka 67. Mapapa wawili wa mwisho, Benedict XVI na Francis walikuwa na umri mkubwa kwa viwango vya karne ya 20 walipoanza upapa wao,” iliripoti CNN.