Nyalandu: Kijana jiulize utaifanyia nini nchi yako

Habari Leo
Published: Oct 21, 2024 11:33:17 EAT   |  Travel

WAZIRI wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewataka vijana nchini badala ya kuuliza nini nchi iwafanyie, ni vema wajiulize wao wataifanyia nini nchi yao. Nyalandu ameyasema hayo, alipohutubia wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana lililopewa jina la Samia Love jijini Mbeya. Amesema taifa la Tanzania litajengwa na Watanzania wenyewe, hivyo ni vema …

The post Nyalandu: Kijana jiulize utaifanyia nini nchi yako first appeared on HabariLeo.

WAZIRI wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewataka vijana nchini badala ya kuuliza nini nchi iwafanyie, ni vema wajiulize wao wataifanyia nini nchi yao.

Nyalandu ameyasema hayo, alipohutubia wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana lililopewa jina la Samia Love jijini Mbeya.

Amesema taifa la Tanzania litajengwa na Watanzania wenyewe, hivyo ni vema kwa vijana kwa pamoja wajiulize nini wataifanyia Tanzania.

Hata hivyo, amesema umuhimu wa swali hilo kwa vijana unatokana na ukweli kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuiweka nchi katika mwelekeo mzuri.

The post Nyalandu: Kijana jiulize utaifanyia nini nchi yako first appeared on HabariLeo.