Njia telezi ya Gachagua kortini akitafuta nyota yake

Taifa Leo
Published: Nov 03, 2024 05:55:04 EAT   |  News

KILA njia ya kisheria aliyopitia aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kujiokoa asing’atuliwe mamlakani iliteleza. Sasa Bw Gachagua 'amerudi kijijini' akisubiri maamuzi mengine ya mahakama iwapo utaratibu wa kumtimua ulikuwa wa kisheria au la. Pamoja na familia yake, Bw Gachagua alipakia picha, Ijumaa baada ya Prof Kithure Kindiki kuapishwa kuwa Naivu Rais, wakiwa wamekalia nyasi kwa tabasamu kubwa katika kiwanja cha makazi yake Mathira, Nyeri. Baadaye Jumamosi Novemba 2,2024 Bw Gachagua alionekana akihudhuria mazishi Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga. Je huu ndio mwisho wa Bw Gachagua kisiasa? Je ana matumaini kujiunga tena na siasa? Sasa, endapo Mahakama zitakubaliana na uamuzi wa Bunge la Seneti wa Oktoba 17,2024 kwamba Bw Gachagua alikiuka maadili na kujihusisha na vitendo vya kuhujumu Katiba basi huu ndio mwisho wake kisiasa. [caption id="attachment_162191" align="alignnone" width="640"] Wakili Paul Muite anayemwakilisha Naibu Rais aliyeondolewa Rigathi Gachagua. Picha|Richard Munguti[/caption] Bw Gachagua atatupwa katika kaburi la sahau kisiasa. Atajiunga na magavana wa zamani Mike Sonko na Ferdinand Waititu ambao sasa hawawezi kuchaguliwa kisiasa au kuteuliwa kutekeleza wadhifa wowote wa umma. Majaribio yote manne ya Bw Gachagua kumzuia aliyekuwa Waziri wa Usalama Prof Kithure Kindiki asiapishwe kuwa Naibu Rais yaligonga mwamba. Majaji watatu wa mahakama ya rufaa Patrick Kiage, Aggrey Muchelule na George Odunga walikataa kuwazuia Majaji Eric Ogola, Antony Mrima na Dkt Freda Mugambi kusoma uamuzi wa kufutilia mbali marufuku ya kuapishwa kwa Prof Kindiki. “Sisi hatuwezi zuia majaji watatu kutoa uamuzi kuhusu uamuzi wa kuzuia Prof Kindiki kuapishwa,” wakasema majaji Kiage, Muchelule na Odunga. Kabla ya kutoa uamuzi huo mawakili wa Bunge la Seneti Prof Tom Ojienda, Wakili wa Prof Kindiki Dkt Muthomi Thiankolu na Bw Michael Muchemi aliyemwakilisha Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse walipinga kesi ya kuwazuia Majaji Ogola, Mrima na Mugambi kutoa uamuzi wao wakisema “hawakupewa nakala za rufaa iliyowasilishwa na Bw Gachagua kupinga kuondolewa kwa marufuku ya kumwapisha Prof Kindiki.” [caption id="attachment_162192" align="alignnone" width="640"] Majaji Antony Mrina , Eric Ogola na Freda Mugambi. Picha| Richard Munguti.[/caption] Majaji Kiage , Muchelule na Odunga walikataa kusitisha kusomwa kwa uamuzi wa kuapishwa kwa Prof Kindiki. Mnamo Oktoba 31, 2024 Majaji Ogola, Mrima na Mugambi waliondoa marufuku ya kuapishwa kwa Prof Kindiki. Mnamo Novemba 1, 2024 Prof Kindiki aliapishwa kuwa Naibu Rais wa tatu tangu katiba ya sasa ipitishwe 2010. Waliomtangulia ni Rais William Ruto, Bw Gachagua na Prof Kindiki. Kuapishwa kwa Prof Kindiki kulifuatia ombi la Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor na mabunge yote mawili kwamba marufuku ya kuapishwa kwa Prof Kindiki yanakinzana na maslahi ya umma. Katika uamuzi wao majaji hao watatu walisema “maslahi ya umma ni kwamba afisi ya Naibu Rais haipaswi kuwa wazi.” Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Prof Githu Muigai na mawakili wa mabunge mawili na maspika Moses Wetang’ula na Amason Kingi walieleza majaji hao hakuna sheria iliyovunjwa kumteua Prof Kindiki kutwaa wadhifa wa Naibu Rais. Prof Kindiki aliteuliwa na Rais William Ruto baada ya Bunge la Seneti kupitisha kutimuliwa kwa Bw Gachagua Oktoba 17, 2024. Bunge la Seneti lilimpata Bw Gachagua na hatia katika mashtaka matano ya kueneza ukabila, hujuma , madharau na kuumbua siri za serikali kwa umma kinyume cha sheria. Baada ya bunge la kitaifa kumpata na hatia Bw Gachagua ilipiga kura na kupitisha hoja ya kumtimua kazini mnamo Oktoba 8, 2024. Uamuzi huo ulipelekwa katika Bunge la Seneti ambapo Bw Gachagua aliamriwa awasilishe ushahidi wa kujitetea dhidi ya madai ya utovu na ukiukaji wa maadili ya kiongozi wa kitaifa na ubaguzi. Bunge la kitaifa lililipokea pendekezo la Rais Ruto la kumteua Prof Kindiki kutwaa wadhifa wa Naibu Rais. Jina lake lilichapishwa katika Gazeti rasmi la serikali. Kabla ya kuapishwa kwa Prof Kindiki kuwa Naibu Rais, Bw Gachagua na walalamishi wengine 30 waliwasilisha ombi katika mahakama kuu wakiomba uteuzi wa waziri huyo wa usalama ufutiliwe mbali. Katika ombi la kumzima Prof Kindiki, Bw Gachagua amedai Naibu Rais huyo mteule hajahitimu kutwaa wadhifa huo kwa vile sio mwanachama wa chama cha kisiasa cha United Democratic Alliance (UDA). Majaji walielezwa Prof Kindiki alijiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu Agosti 9 2022 kuwa mwanachama wa UDA Mawakili Paul Muite, Prof Elisha Ongoya, Tom Macharia (wanaomwakilisha Gachagua)  na Jackson Kala anayewakilisha chama cha Wiper waliomba korti ikubaliane na maamuzi ya Majaji Richard Mwongo na Chacha Mwita kwamba uteuzi wa Prof Kindiki unakinzana na mwongozo wa Katiba kuhusu uteuzi. [caption id="attachment_162193" align="alignnone" width="640"] Majaji Antony Mrima ,Eric Ogola na Dkt Freda Mugambi waliotoa marufuku ya kumwapisha Prof Kithure Kinduki. Photo|Richard Munguti[/caption] Mabw Muite na Macharia walieleza Majaji Ogola, Mrima na Mugambi kwamba uteuzi wa Prof Kindiki wapasa kukataliwa kwa vile haujaidhinishwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC). “Hakuna makamishna wa IEBC na kwamba uidhinishwaji wa Prof Kindiki na IEBC na tume huru ya kupambana na ufisadi (EACC) umekinzana na katiba,” walisema mawakili Muite, Macharia pamoja na wakili wanaowakilisha Diwani Benjamin Munyi Mathenge. Mathenge anawakilishwa na mawakili Kibe Mungai na Ndegwa Njiru. Wakili Teresia Wanjiru na walalamishi wengine 27 wamelalamika kwamba Bw Gachagua hakuondolewa afisini kwa njia inayofaa. Mahakama iliombwa na Bw Gachagua isitishe uteuzi wa Prof Kindiki kwa vile hajajiuzulu wadhifa wa Uwaziri. Pia wamelalama maoni ya wananchi hayakukusanywa kabla ya kuteuliwa kwa Prof Kindiki. Lakini Prof Githu Muiga, Prof Tom Ojienda na mawakili Ben Millimo, Peter Wanyama, Paul Nyamodi, Dkt Muthomi Thiankolu na Eric Gumbo waliomba mahakama iamuru Prof Kindiki aapishwe kwa vile aliteuliwa kwa mujibu wa sheria. Prof Ojienda alieleza majaji hao kwamba “uamuzi wa Gachagua kubanduliwa mamlakani na Bunge la Seneti hauwezi kubatilishwa na mahakama kuu.” Mawakili Prof Muigai, Prof Ojienda na mawakili Millimo, Nyamodi na Wanyama walisema mahakama kuu haina uwezo wa kubatilisha uamuzi wa Bunge la Seneti na kwamba “ Bw Gachagua afungashe virago aende nyumbani - hawezi kupata msaada na usaidizi kortini.” Dkt Thiankolu alisema mahakama kuu haiwezi kuhoji uamuzi wa suala la Rais na Naibu Rais ila Mahakama ya Juu tu. “Ni Mahakama ya Juu tu iliyotunukiwa mamlaka ya kujadilia suala la nyadhifa za Rais na Naibu Rais.Futilieni mbali maagizo ya Majaji Mwita na Mwongo ya kusitisha kuapishwa kwa Prof Kindiki kutwaa wadhifa wa Naibu Rais,”Dkt Thiankolu alisema. Majaji hao walielezwa na Prof Muigai kwamba maamuzi ya Majaji Mwita na Mwongo yametumbukiza nchi hii katika utata wa kikatiba kwa vile “nchi haina Naibu Rais na Waziri wa Usalama.” Majaji hao waliombwa wasisite kutekeleza sheria jinsi ilivyo kwa kuamua hawana mamlaka ya kuamua iwapo Bw Gachagua aling’atuliwa mamlakani kwa mujibu wa sheria.