Ni huzuni Simba SC

ZANZIBAR; NI huzuni kwa mashabiki wa Simba na Watanzania kwa ujumla baada ya leo Mei 25, 2025 kushuhudia timu Simba ikishindwa kutwaa ubingwa katika mchezo wa marudiano fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya timu hiyo na RS Berkane ya Morocco. Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa New …
ZANZIBAR; NI huzuni kwa mashabiki wa Simba na Watanzania kwa ujumla baada ya leo Mei 25, 2025 kushuhudia timu Simba ikishindwa kutwaa ubingwa katika mchezo wa marudiano fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya timu hiyo na RS Berkane ya Morocco.
Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, hivyo kushuhudia ubingwa wa Kombe la Shirikisho ukienda Morocco.
Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 mfungaji akiwa Joshua Mutale, kabla ya Berkane kusawazisha dakika ya 90+3 mfungaji akiwa Soumaila Sidibe.