JARIBIO la kumuua Naibu Gavana wa Homa Bay Oyugi Magwanga lilitekelezwa Jumapili usiku.
Hii ni baada ya watu wasiojulikana na ambao walikuwa na bunduki kusemekana kujaribu kumpiga risasi Bw Magwanga alipokuwa akielekea nyumbani mwendo wa saa tatu na nusu usiku.
Lakini walinzi wake walitibua njama hiyo kwa kuwafyatulia risasi wahalifu hao.
Kisa hicho kimetokea siku 11 pekee baada ya Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were kuuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi.
Isitoshe, diwani mmoja kutoka eneo bunge hilo, Vickins Bondo (anayewakilisha Wadi ya West Kasipul) aliripoti kuwa alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi akiwa Nairobi.
Bw Magwanga, ambaye pia anatoka eneo bunge la Kasipul, sasa anasema kuwa maisha yake yamo hatarini kufuatia kisa hicho cha Jumapili ambapo majambazi walilenga kumuua.
“Nimekuwa nikipokea vitisho lakini sijawahi kuvichukulia kuwa na uzito. Sasa ninahofia usalama wangu,” naibu huyo wa gavana akaeleza.
Bw Magwanga amewahi kuhudumu kama Mbunge wa lililokuwa eneo bunge la Kasipul Kabondo kati ya 2007 na 2013.
Kisha eneo bunge hilo liligawanywa na Bw Magwanga akachaguliwa kuwa Mbunge wa Kasipul. Naibu huyo wa Gavana anaishi katika kijiji cha Kabuor.
Mnamo Jumapili alipokuwa akirejea nyumbani alipata habari kwamba watu fulani, wenye malengo yasiyojulikana, walikuwa wakimwandama.
“Nilipata habari za kijasusi kwamba watu fulani walikuwa wakinifuata Jumapili usiku. Nililazimika kuchukua hatua za haraka,” Bw Magwanga akasema.
Afisa huyo wa serikali ya kaunti ya Homa Bay, aliamua kutumia njia tofauti kufika nyumbani alipogundua kuwa watu fulani walikuwa wakimfuata.
Kama kawaida, gari la Bw Magwanga hutumia barabara ya Oyugis kuelekea Sondu kabla ya kufika katika kituo cha kibiashara cha Mathenge kilichoko hatua chache kutoka nyumbani kwake.
Wakati wa tukio hilo, gari lake lilielekezwa upande Gamba, lilipotoka Oyugis Mjini kabla ya kuingia katika barabara nyingine inayoelekea nyumbani kwake.
“Nilikuwa nimewaeleza wale walikuwa nyumbani kwamba wawe tayari kunifungulia lango ili niingie kwenye boma haraka. Walinzi wangu pia walikuwa na habari kwamba kundi la majambazi lilikuwa likinifuata,” akaeleza.
Hivyo ndivyo, Bw Magwanga alifaulu kukanganya wahalifu ambao walikuwa wakipanga kumshambulia.