Mzee yusuph ajivunia muziki wa taarabu
MSANII wa muziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph ‘Mfalme wa Taarabu’ anatarajia kupewa mauwa yake kwa kuupigania muziki…
The post Mzee yusuph ajivunia muziki wa taarabu appeared first on HabariLeo.
MSANII wa muziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph ‘Mfalme wa Taarabu’ anatarajia kupewa mauwa yake kwa kuupigania muziki huo katika tamasha la la muziki huo linalotarajia kufanyika Disemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na habarileo Mzee Yusuph amesema kuwa watu wengi wanapenda kuwapa watu mauwa yao wakiwa wametangulia mbele za haki kwangu ni tofauti.
“Napewa mauwa yangu na ninayapokea kwa sababu najuwa kuwa nastaili maua haya, nimefanya muziki wa taabu kwa muda Mwingi lakini hakuna mwanaume yupo muda mrefu kwenye huu muziki zaidi yangu.
“Kuna muda muziki wa taarabu ulikuwa kama umelala hakuna anayeweza kuuamsha kama Mzee Yusuph niwaambie tu watu wajitokeze kwa wingi Disemba 8 waone muziki unavyozaliwa upya huku nikipokea mauwa yangu.”amesema Mzee Yusuph
Aidha ameongeza kuwa atahakikisha muziki wa amapiano unaingia upya katika Tasnia ya Taarabu kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye muziki huo pendwa.
The post Mzee yusuph ajivunia muziki wa taarabu appeared first on HabariLeo.