Mwijaku kuhojiwa sakata la wanafunzi wa chuo

DAR ES SALAAM; SERIKALI imesema kijana aitwaye Mwijaku aliyetajwa kwenye video fupi kuhusu sakata la wanafunzi wa vyuo…
The post Mwijaku kuhojiwa sakata la wanafunzi wa chuo appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAM; SERIKALI imesema kijana aitwaye Mwijaku aliyetajwa kwenye video fupi kuhusu sakata la wanafunzi wa vyuo vikuu kumdhalilisha mwenzao, atahojiwa na Polisi.
“Ndugu wananchi, rejeeni taarifa yangu kwa umma ya tarehe 20 Aprili, 2025 kuhusu mada tajwa hapo juu. Jeshi letu la Polisi linaendelea kutimiza wajibu wake wa kisheria kuhusu kuwahoji wahusika wa tukio hilo.
“Aidha, kwa upande mwingine, jamii nayo imeendelea kuhoji mbona aliyetajwa kuwa ni Mwijaku hakamatwi?
“Ndugu Wananchi, napenda kuwahakikishia kuwa, Mwijaku aliyetajwa kwenye video za mgogoro wa mabinti hao, naye atahojiwa kwa mujibu wa sheria na baada ya hapo, wizara yangu itaona nini ifanye kuhusu mustakabali mzima wa maadili ya jamii na nafasi ya huyo Mwijaku na wengine wote wenye nafasi zenye kuchochea kasi ya athari chanya au hasi kwenye maadili ya jamii,” imesema taarifa ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalumu, Dorothy Gwajima.
The post Mwijaku kuhojiwa sakata la wanafunzi wa chuo appeared first on HabariLeo.