Mwenge kumulika miradi 6 Mtwara Mikindani

Habari Leo
Published: May 25, 2025 10:50:45 EAT   |  General

MTWARA; MWENGE wa Uhuru 2025 leo umeingia katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kumulika miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 955. Mkurungezi wa Manispaa hiyo Mwalimu Nyange, amesema hayo wakati akipokea Mwenge huo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na kueleza kuwa utakimbizwa kilometa 42 kukagua na kuzindua miradi minne, kuweka …

MTWARA; MWENGE wa Uhuru 2025 leo umeingia katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kumulika miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 955.

Mkurungezi wa Manispaa hiyo Mwalimu Nyange, amesema hayo wakati akipokea Mwenge huo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na kueleza kuwa utakimbizwa kilometa 42 kukagua na kuzindua miradi minne, kuweka jiwe la msingi mradi mmoja na mradi mwingine utakaguliwa.

Miradi ambayo itamulikwa na kuzinduliwa ni mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa, ujenzi wa kisima Cha maji, uzinduzi wa Jengo la redio ya Jamii HFM.

Miradi mingine ambayo itamulikwa ni mradi wa ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje katika zahanati ya Mtwawanya , na mradi wa uzalishaji wa malighafi za ujenzi.