Mwanamuziki Princess Jully maarufu kwa kibao ‘Ukimwi Mbaya’ aaga dunia

Taifa Leo
Published: Oct 12, 2024 16:41:37 EAT   |  Entertainment

MWANAMUZIKI mashuhuri wa mtindo wa Benga Princess Jully amefariki.

Mwanamuziki huyo (jina halisi Juliana Auma) maarufu kwa kibao chake, “Dunia Mbaya” alifariki Jumamosi, Oktoba 12, 2024, katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Migori ambako amekuwa akipokea matibabu kwa kipindi cha miezi miwili.

Isipokuwa kibao "Dunia Mbaya" Pricess Jully aliimbia nyingi zake zingine kwa lugha yake asilia, dholuo.

Mmoja wa wanawake wa kiume Bradley Ogudah aliambia Taifa Dijitali kwamba mamake alipoteza ufahamu mwendo wa asubuhi kabla ya kukata roho mwendo wa saa nane za mchana.

“Amekufa. Amekuwa akiugua kwa miezi miwili,” akaeleza.

Princess Jully, 51, alipata umaarufu  kati ya miaka ya 1990 na 2000 kutokana na kibao hicho “Dunia Mbaya” kinachosheheni maudhui ya kuonya watu dhidi ya kuambukizwa ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Marehemu ni mke wa tatu wa marehemu Jully Okumu (Prince Jully), mwanamuziki aliyechomoa vibao “Malo Malo” (Juu Juu) na “Akuru” (Njiwa), miongoni mwa vingine.

Prince Jully alikuwa mwanzilishi wa bendi ya  Jolly Boys band, alikufa mnamo 1997.