Muhas yaja na mkakati kukabili usonji

Habari Leo
Published: Apr 09, 2025 03:04:14 EAT   |  Educational

DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kitaendelea kuzalisha wataalamu wa shahada…

The post Muhas yaja na mkakati kukabili usonji appeared first on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kitaendelea kuzalisha wataalamu wa shahada ya awali ya mazoezi ya viungo ‘Physiotherapia’ kufundisha matamshi ‘speech therapy’ kusaidia wenye hali ya usonji.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mkurugenzi wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Afya na Akili kutoka Wizara ya Afya, Dk Omary Ubugoyu, amesema wataendelea kufanya ufumbuzi kugundua wenye usonji ili wafikishe hospitalini.

Akizungumza katika kongamano la kitafiti linalojadili hali ya usonji  lililofanyika chuoni hapo leo April 9, 2025, Dar es Salaam, Dk Ubugoyu amesema ufumbuzi huo utafanyika hospitalini na maeneo mengine ili kuwachukulia hatua za haraka wahusika wa hali ya usonji.

Amesema kuwa wanaongeza idadi ya wahudumu wa afya katika hospitali za ngazi za rufaa za mikoa waweze kuwatambua wagonjwa, huku akieleza  Mkoa wa Dar es Salaam kuna shule za awali  100 na walimu 4,000 ambao watafundishwa namna ya kumgundua mtoto mwenye usonji.

“Serikali ina mkakati wa kuongeza watoa huduma wa matibabu bingwa ambao watakuwa wataalamu wa tiba ya viungo,  kazi,  saikolojia na matamshi,” amesema Dk Ubugoyu.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema moja ya jukumu kubwa ni kuwafundisha watoa huduma za afya na kufanya tafiti lengo kuzalisha wataalamu kukabiliana na changamoto hizo.

“Mapendekezo tunayotoa ni kuwasaidia watunga sera kufanya maboresho, wazazi na jamii namna ya kuishi nao na kuacha kuwanyanyapaa,” amesema Profesa Kamuhabwa.

Profesa Bruno, Sunguya Mkuu wa Idara ya Utafiti MUHAS, ametaja dalili za hali hiyo kuwa ni mtoto au mkubwa kushindwa kuwasiliana, kujitenga na wenzake.

 “Mtoto mwenye usonji sio mlemavu na kwamba anaweza kubadilika mapema akipatiwa matibabu mapema,” amesema Profesa Bruno Sunguya.

Amesema kuwa tatizo la usonji limekuwa likiongezeka, kumetokana na ungezeko la wataalamu ambao wanauwezo wa kutambua ugonjwa huo.

Aidha, Daktari Bigwa wa Watoto, Profesa Karimu Manji, amesema ameonya tabia ya wazazi wengi kuacha utaratibu wa kuwalea watoto katika mazingira ya matumizi ya televisheni, simu na vingine.

“Screen time  kwa watoto chini  ya miaka mitano ni hatari sana, mzazi jaribu kufuatilia,  katuni kwa kumuelekeza mtoto kila kinachofanywa na namna kinavyotamkwa, kuwe na ufundishaji na sio kumtelekezea mtoto aangalie mwenyewe ili kumnyamazisha si sahihi,” amesema Profesa Manji.

 “Tusiwanyanyapae watoto hawa na tiba yao ni kuwagundua mapema na kuanza kuwapatia tiba ya matamshi na viungo ambazo gharama yake ni kubwa kwa siku ni 100,000 na kwa vile ni endelevu, wazazi wanafilisika tunahitaji mkakati wa makusudi katika sera zetu,” amesema Profesa Manji.

The post Muhas yaja na mkakati kukabili usonji appeared first on HabariLeo.