Minyoo wekundu kuunda mbolea asilia

ALIPOKAMILISHA masomo ya Shule ya Upili mwaka 2014, George Muturi alijitosa kwenye ufugaji wa kuku kujiendeleza kimaisha.
Barobaro huyu, vilevile, alikuwa akifuga sunngura angaa kuongeza mapato.
Hata hivyo, gharama ya malisho ikizingatiwa kuwa ghali alikuwa hajajijenga kifedha na nusra izime ndoto zake.
Alijikuna kichwa jinsi angeangazia changamoto hiyo, na kupitia utafiti aliofanya mitandaoni akapata jawabu.
“Chakula kilichosheheni virutubisho vya Protini ni muhimu sana kwa kuku hasa kwa lengo la mayai na nyama. Kupitia intaneti, nilibaini ufugaji wa minyoo wekundu (red earthworms), ndio bora zaidi,” Muturi anaelezea.
Wadudu hao wenye tija chungu nzima, wanafugwa kupitia teknolojia inayofahamika kama Vermiculture.
[caption id="attachment_168429" align="aligncenter" width="300"] George Muturi, mkulima katika Kaunti ya Kiambu akielezea anavyotengeneza mbolea asilia kwa kutumia wadudu wekundu wa ardhini. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption]
Kupata wadudu wa kuanzisha safari, Muturi anakiri haikuwa mteremko.
Shukran kwa mfugaji katika Kaunti ya Kiambu aliyemuokoa.
Alianza na mtaji wa Sh10, 000, kilo moja ya minyoo hao wenye thamani akiuziwa Sh1, 000, hela alizosaidiwa na mamake.
“Nilianza na kizimba kikuukuu cha sungura chenye ukubwa wa futi 10 kwa 10,” anasema.
Huduma zake wakati huo, alikuwa akiziendesha chini ya Agritech Organic Farm.
Mwaka wa 2018, miaka minne baada ya kuhitimu kidato cha nne, Muturi aliamua kubadilisha taswira ya biashara yake.
“Badala ya kuegemea sana kuzalisha minyoo wa kulisha kuku, tualianza kuwatumia kuunda mbolea ya kiasili,” anasema.
[caption id="attachment_168430" align="aligncenter" width="300"] Masanduku yenye wadudu wekundu kuunda mbolea asilia. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption]
Anadokeza kwamba, ushawishi huo ulitokana na jinsi alivyoona wakulima wakihangaika kupata mboleahai au mbolea ya asili kukuza chakula salama.
Mawazoni, Muturi alikuwa na imani kuwa gapu hiyo angeiziba.
Hivyo ndivyo Comfort Worms and Insects ilivyozaliwa, kampuni ya kijana mwenye umri wa 30 inayofanya makuu nchini.
Anatumia wadudu hao kuunda mboleaasilia.
Aidha, huwalisha majani na matawi ya mimea, ikiwa ni pamoja na taka za sokoni; mazao mabichi ya shambani.
“Masalia ya chakula kilichopikwa hayatumiki kwa sabau yamepitia taratibu za kuangamiza virutubisho muhimu kwa minyoo,” anatahadharisha.
Vilevile, hutumia kinyesi cha mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe.
[caption id="attachment_168432" align="aligncenter" width="300"] George Muturi hutumia kinyesi cha mifugo na masalia ya mimea kufuga minyoo wanaotumika kuunda mbolea asilia.[/caption]
Kisichotumika, ni cha kuku Muturi akisema kina kiwango cha juu cha Amonia.
Anapokusanya masalia hayo ya mimea, taka na vinyesi, vyote vikipaswa kuwa na unyevuunyevu, huviweka kwenye masanduku aliyounda kuanza safari kutengeneza mbolea.
Ana jumla ya masanduku 300, na ndani - chini yake huweka nyasi zilizokauka kabla ya kinyesi, mimea na taka kuwekwa, vyote vikiwa ndio chakula cha minyoo hao.
“Kinachofuata, ni kuweka wadudu hao ili waanze shughuli ya kuunda mbolea kwa kula malighafi hayo, na kuyageuza kuwa bidhaa muhimu katika kilimo,” anafafanua.
Inachukua siku 60, sawa na miezi miwili, mbolea ya asili kuwa tayari. Mbolea ni kinyesi cha minyoo hao.
Muturi ana mtambo wa kuchuja, kutenganisha mbolea, na vipande vikubwa vya malighafi yaliyosalia, na vilevile minyoo.
[caption id="attachment_168431" align="aligncenter" width="300"] Mtambo maalum wa kuchuja minyoo na mbolea ambayo George Muturi hutengeneza. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption]
Kulingana na mjasiriamali huyu bunifu, mfuko wa kilo 50 huuza Sh1, 500, kilo 30 Sh1, 500 na kilo 10, Sh600.
Ana wateja wakulima wanaothamini kilimohai kutoka Kaunti ya Kiambu, Nakuru, Nairobi, Machakos, Murang’a, na Embu.
Kutoka mradi wenye kipimo cha futi 10 kwa 10, sasa anajivunia biashara kupanuka na kukalia kipande cha ardhi chenye ukubwa wa futi 50 kwa 60, katika eneo la Kagaa, Lari, Kaunti ya Kiambu.
Alianza na mfanyakazi mmoja, na sasa ana jumla ya saba; wa kudumu na vibarua.
Muturi pia ni mfugaji hodari, wakati wa mahojiano shambani mwake tukimpata akiwa na kuku wapatao 200, samaki akikadiria kuwa 2, 000 na sungura 70.
[caption id="attachment_168433" align="aligncenter" width="300"] Mbolea asilia tayari kuelekezwa shambani. PICHA|SAMMY WAWERU[/caption]
Kando na kutumia wadudu hao kulisha kuku na samaki, vile vile ana wengine wanaojulikana kam Black Soldier Fly (BSF) na pia hukuza Azolla.
Anakadiria kupunguza gharama ya malisho kwa karibu asilimia 30.
Anasema ufanisi wake umetokana kwa ajili ya kushirikiana na mashirika kama NGO na taasisi za kiserikali, ikiwemo Wizara ya Kilimo na Ustawishaji Mifugo, la muhimu zaidi likiwa kutafiti kuboresha biashara yake.