Mimi sio ‘mjanja’, naponea kutokana na neema ya Mungu, Ruto ajitetea kanisani

RAIS William Ruto amekana madai kuwa yeye ni kiongozi mjanja anayefahamu njia za kukwepa misukosuko ya kisiasa na matukio yanayotishia kuangamiza serikali yake, kila mara.
Akirejea kichwa cha habari kuu katika gazeti la The Sunday Standard toleo la Jumapili, Machi 2, 2025, Cunning Ruto (Ruto mjanja), Dkt Ruto alisema kuwa ni neema ya Mungu inayomwezesha kuponea changomoto hizo.
“Ukisoma gazeti moja la leo, kichwa cha habari kinasema kuwa Ruto ni mjanja zaidi. Nataka kuwaeleza kuwa mimi sio mjanja wanavyofikiri. Hii ni neema ya Mungu inayoniongoza. Tunamwamini Mungu,” akasema alipohudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la Jesus Winner Ministry, lililoko Roysambu, Nairobi.
“Kwa sababu nilikwepa mitego niliyowekewa, wanasema mimi ni njanja. Hiyo sio kweli, nafanya tu kile ambacho Abrahamu alifanya kama inavyoelezwa katika Bibilia. Aliamini Mungu wakati mambo yalikuwa magumu. Siyo yale mnayosema, ni neema ya Mungu kwa taifa hili.” akakariri.
Rais Ruto aliorodheshwa mafanikio ya serikali yake katika sekta za kilimo ambayo yamechangia ongezeko la uzalishaji wa mahindi, majani chai, kahawa, miwa miongoni mwa mazao mengine.
Hata hivyo, Rais Ruto aliungama kuwa mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) inayotekeleza bima mpya ya afya ya kijamii (SHIF) inakabiliwa na changamoto hali inayochangia wagonjwa wengi kukosa huduma.
“Ni kweli kwamba SHA inakabiliwa na changomoto katika kufanikisha mpango wetu wa kutoa huduma za afya kwa wote. Lakini nawaomba Wakenya muda lakini ninawakikishia kuwa mpango huo wa bima ufaulu. Hilo ndilo lengo la serikali na niko na uhakikisha kuwa tutalitimiza,” Dkt Ruto akawaambia waumini katika Kanisa hilo.
Rais Ruto alisema hayo kufuatia malalamishi kutoka kwa wagonjwa wanaolazimika kulipa pesa taslim kugharamia huduma zao za matibabu baada ya kufeli kwa mfumo wa SHA.
Aidha, hospitali za kibinafsi zinazotoa huduma za afya katika maeneo ya vijijini na mijini zimesitisha utoaji huduma kwa wenye bima inayosimamiwa na SHA baada ya serikali kulipa malimbikizi ya madeni ya Sh30 bilioni.