Mil 348/- kuwezesha mikopo halmashauri Iramba

Habari Leo
Published: Oct 20, 2024 10:29:58 EAT   |  Business

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda amewataka vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya biashara ili kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri. DC Mwenda ameyasema hayo Oktoba 19,2024 alipofanya ziara kwenye vijiji vya kata ya Kidaru, akijibu swali lililoulizwa na Anderson Naligia kutoka Kidaru aliyetaka kujua ni …

The post Mil 348/- kuwezesha mikopo halmashauri Iramba first appeared on HabariLeo.

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda amewataka vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya biashara ili kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri.

DC Mwenda ameyasema hayo Oktoba 19,2024 alipofanya ziara kwenye vijiji vya kata ya Kidaru, akijibu swali lililoulizwa na Anderson Naligia kutoka Kidaru aliyetaka kujua ni lini serikali itawaajiri vijana wao kwani wamewasomesha kwa kuuza mifugo yao na bado hawajaajiriwa wapo mtaani.

Akijibu swali hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imejipanga kutenga zaidi ya Sh milioni 348.969 kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo inayotoka na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri.

“Tuna Vijana zaidi ya 25000 wilayani Iramba, serikali inaendelea kutoa ajira, niwaombe tuwafundidhe vijana watengeneze vikundi kwa ajili ya kupatiwa mikopo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali wanazozifanya katika maeneo yao,”amesema DC Mwenda

Aidha Mwenda amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kurejesha mikopo ya asilimia 10 toka alipositisha mikopo hii mwezi wa nne mwaka 2023.

The post Mil 348/- kuwezesha mikopo halmashauri Iramba first appeared on HabariLeo.