Mhe. Prof. Kitila Mkumbo aipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania

Milard Ayo
Published: Oct 22, 2024 06:25:46 EAT   |  News

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza ufanisi wa kuhudumia Shehena mbalimbali katika Bandari zake hususani Bandari ya Dar es Salaam, kufuatia uwekezaji wa Wabia kampuni ya DP World na East Africa Gateway Terminal LTD (EAGTL). Profesa Mkumbo ametoa […]

The post Mhe. Prof. Kitila Mkumbo aipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania first appeared on Millard Ayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza ufanisi wa kuhudumia Shehena mbalimbali katika Bandari zake hususani Bandari ya Dar es Salaam, kufuatia uwekezaji wa Wabia kampuni ya DP World na East Africa Gateway Terminal

LTD (EAGTL).

Profesa Mkumbo ametoa pongezi hizo tarehe 21 Oktoba, 2024, alipotembelea Makao Makuu ya TPA na Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea Shughuli za Utekelezaji zinavyofanyika Bandarini hapo kwa ushirikiano na Wabia na namna Uwekezaji huo utakuwa na tija na kuongeza ufanisi katika huduma za Bandari Nchini pamoja na kuchangia Pato la Taifa.

“Nimefurahishwa na maboresho makubwa ya kimiundombinu na utendaji kazi katika Bandari za TPA hususani Bandari hii Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa Wawekezaji, maboresho haya yana lengo chanya na imani yangu ni kuwa Uwekezaji huu utakuwa na tija na kuongeza ufanisi zaidi katika huduma za Bandari Nchini na kuchangia Pato la Taifa”. Amesema Mhe.Prof. Mkumbo.

Mhe. Profesa Mkumbo amesema ziara yake hiyo kutembelea Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa ajili ya Maandalizi ya Mipango ya Nchi kwa Mwaka ujao wa fedha na mipango ya maendeleo ya Taifa inayoongozwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha Mhe. Prof.Mkumbo ameipongeza Bodi na Menejimenti ya TPA kwa usimamizi mzuri katika Bandari Nchini hali inayopelekea Uchumi wa Nchi kukua na kutoa wito kwa Wawekezaji wanaoendesha Terminal 1 na 2 katika Bandari ya Dar es Salaam DP World na EAGTL, kuhakikisha wanatekeleza makubaliano yaliyomo kwenye Mikataba yao Kwani Serikali inamatarajio makubwa kutoka kwao na Kwamba itahakikisha inasimamia kikamilifu uwekezaji huo ili uendelee kuleta tija katika Taifa

The post Mhe. Prof. Kitila Mkumbo aipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania first appeared on Millard Ayo.