Mfumo wa kisheria wa kusimamia mikataba ya kabla ya mdoa Kenya

Taifa Leo
Published: May 11, 2025 06:00:09 EAT   |  News

Kifungu cha 40(1) cha Katiba ya Kenya ya 2010 kinabainisha kuwa kila mtu ana haki ya kumiliki mali peke yake au kwa ushirikiano katika sehemu yoyote ya Kenya.

Kifungu cha 40(2)(b) kinakataza sheria yoyote itakayoruhusu serikali au mtu yeyote kuzuia au kuingilia haki hizi kwa misingi ya hali ya ndoa, kama ilivyoelezwa kwenye Kifungu cha 27(4).

Kifungu cha 6(3) cha Sheria ya Mali ya Ndoa kinawaruhusu wanaotarajia kufunga ndoa kuingia kwenye makubaliano kuhusu mali zao kabla ya ndoa. Hata hivyo mkataba wa kabla ya ndoa unaweza kufutwa na mahakama. Kifungu cha 6(4) cha Sheria hii kinapatia mahakama mamlaka ya kufuta mkataba huu iwapo itathibitika kuwa ulifanyika kwa udanganyifu, shinikizo au haukuwa wa haki kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, Sheria haielezi kwa undani maana ya udanganyifu, shinikizo au mkataba usio wa haki na hii itakuwa kazi ya mahakama kupima mawasilisho ya pande zote kabla ya kutoa uamuzi. Kwa kuwa sheria ya Kenya haizungumzi moja kwa moja mikataba ya baada ya ndoa (post-nuptial agreements), pengo linaibuka. Hata hivyo, mahakama zimechukua hatua kushughulikia nafasi ya mikataba hii katika ndoa zilizopo.

Katika kesi moja CYC dhidi ya KSY (2014), Mahakama Kuu ilithibitisha na kurejelea mkataba wa baada ya ndoa uliosainiwa na pande zote katika kuamua ombi la mlalamishi kuhusu matunzo ya muda.

Katika kesi nyingine OKN dhidi ya MPN (2017) Mahakama ya Rufaa ilieleza kuwa chini ya Kifungu cha 17(1) cha Sheria ya Ndoa, mahakama ina uwezo wa kuamua ugavi wa mali baada ya ndoa kuvunjwa, na kwamba inaweza kuchunguza mikataba ya kabla au baada ya ndoa iliyofanywa na wanandoa. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria na maamuzi ya mahakama, wanandoa wanaotafakari kusaini mkataba wa kabla ya ndoa wanapaswa kuzingatia  masuala ya matunzo ya watoto yazingatiwe kabla ya kusaini mkataba huu, kwani haki za mtoto zina nafasi ya kwanza chini ya sheria ya Kenya. Kama ilivyoamuliwa katika kesi ya Radmacher dhidi ya Granatino (2010) mkataba hauwezi kuathiri mahitaji halali ya mtoto yeyote wa familia.

Kama nilivyoeleza katika makala ya wiki jana, ingawa hakuna muda maalum uliowekwa chini ya Sheria, sheria ya kawaida inapendekeza mkataba huu usainiwe chini ya siku 21 kabla ya ndoa.

Pande zote zinapaswa kutafuta ushauri wa kisheria huru kabla ya kutia saini mkataba wa kabla ya ndoa, kuthibitisha kuwa waliingia kwenye mkataba kwa hiari na bila kudanganywa au shinikizo. Kwa mfano, katika kesi ya DB dhidi ya PB (2016) EWHC 3431 (fam), dai la mke kuhusu kupotoshwa halikufaulu kwani ilibainika alipata ushauri huru wa kisheria.

Hatimaye, mkataba unaweza kurekebishwa kwa kuongeza, kuondoa au kusahihisha vipengele, lakini marekebisho hayo lazima yafanyike kwa maandishi na kwa ridhaa ya pande zote mbili.