Mchechu achangisha mil 117.8/- ujenzi wa kanisa

Habari Leo
Published: Oct 21, 2024 08:04:31 EAT   |  Business

KILIMANJARO : Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu ameendesha harambe iliyowezesha kuchangisha Sh milioni 117.8 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Naibili, Siha, Kilimanjaro. Kati ya fedha hizo kwa ajili ya jengo jipya la ibada ambalo ujenzi wake ulianza miaka sita iliyopita. Katika harambe hiyo iliyofanyika jana …

The post Mchechu achangisha mil 117.8/- ujenzi wa kanisa first appeared on HabariLeo.

KILIMANJARO : Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu ameendesha harambe iliyowezesha kuchangisha Sh milioni 117.8 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Naibili, Siha, Kilimanjaro.

Kati ya fedha hizo kwa ajili ya jengo jipya la ibada ambalo ujenzi wake ulianza miaka sita iliyopita. Katika harambe hiyo iliyofanyika jana katika Usharika huo pia ilipatikana mifuko 118 ya saruji.

Pesa hizo na saruji ni kwa ajili ya upauzi wa jengo hilo la ibada na kazi ya plasta, kwa mujibu wa Askofu Dk. Fredrick Shoo, Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT.

Kazi hizo mbili za upauzi na plasta, zinatarajiwa kugharimu kiasi cha Sh milioni 150. Akizungumza na viongozi wa kidini, serikali na kijamii, pamoja na waumini wa Naibili, Mchechu alieleza haja ya kuendelea kuwa na moyo wa kutoa na kushirikiana mpaka ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada utakapokamilika.

Kwa sasa tayari jiwe la pembe limewekwa katika kanisa hilo. Mchechu aliwataka wakristo kutoishia kwenye hatua hiyo ya kuweka Jiwe la Pembe tu.

“Tunapoendelea na ujenzi huu, nataka niwaombe ninyi wapendwa msiishie hapa. Tuendelee kufanya kazi kwa pamoja mpaka ujenzi utakapokamilika,” amesema.

Kwa upande wa Dk.Shoo, amesema matamanio yao ni kuona wanakamilisha plasta, kuweka madirisha, milango na madhabahu, kupaka rangi na kuanza maandalizi ya kutengeneza samani, ifikapo mwaka 2026.

Mpaka kufikia hatua ya kabla ya upauzi, jumla ya kiasi cha Sh milioni 229.8 kimetumika, shukrani kwa watu wenye mapenzi mema na Mungu kwa michango yao.

The post Mchechu achangisha mil 117.8/- ujenzi wa kanisa first appeared on HabariLeo.